Ni mara ngapi umelisikia hili neno, Fast Charge/Quick Charge? .. natumai ni mara nyingi tuu..lakini je wengi wetu tunajua maana yake?
Ni wazi kuwa Simu Janja nyingi huwa zinasapoti teknolojia ya Fast Charging na huwa ni moja kati ya vipengele vya kuiweka juu simu husika na kutofautisha na zingine.
Sasa Basi Fast Charging Ni Nini?
Kwa haraka haraka ni kwamba hii ni teknolojia ambayo inakuwezesha kuweza kujaza betri la Simu Janja yako kwa haraka kadri inavyowezekana.
Yaani chaja itavuta umeme mwingi (kwa usalama kabisa) kutoka katika chanzo na kuupeleka katika simu yako. Hili litafanyika wakati simu janja na charge yako vyote vinaruhusu hili.. Mfano ukiwa na chaji ambayo inasapoti teknolojia hii lakini simu janja yako ikawa haisapoti basi hutapata huduma hii.
Teknolojia hii kwa mara ya kwanza kabisa ililetwa na kampuni ya Qualcomm chini ya kitengo cha Snapdragon amacho ndio kitengo maalum cha kutengneza chip mbali mbali.
Chip hizi zikikaa katika kifaa (simu janja) na ukifanikiwa kupata chaja inayosapoti teknolojia ya ‘fast charging’ bila shaka simu yako itaweza ingiza charge kwa haraka zaidi.
Qualcomm wenyewe walisema kuwa kwa kutumia teknolojia yao ..simu inaweza kujaa kwa 75% zaidi ya chaja za kawaida.
Kumbuka chaji nyingi katika soko huwa zinakubali 5V 1A, lakini za Qualcomm zinaenda mpaka 5V, 9V au 12V (volt) na kufika mpaka 3A (Ampere).
La Muhimu ni kwamba simu janja iwe inaruhusu teknolojia hii na pia chaja yako iwe inaruhusu teknolojia hii.
Vile vile Qualcomm sio mtengenezaji pekee wa teknolojia hii kuna wengine wengi tuu, lakini yeye ni maarufu zaidi.