Fahamu: Simu Janja 1000 zinaingia Sokoni kwa Kila Sekunde 21.8

0
Sambaza

Data zinazoendelea kuwekwa wazi katika mkutano mkubwa wa teknolojia za mawasiliano mjini Barcelona huko Hispania unaonesha jinsi gani kuna maendeleo makubwa sana katika sekta hii muhimu.

Kuna maendeleo yanayovutia sana duniani kote hasa kwenye nyanja ya simu na utumiaji wa teknolojia ya intaneti.B_BoAguXEAA-A08

Fahamu haya machache;

1. Kuna takribani ya simu janja elfu 1 zinaingia sokoni kila baada ya sekunde 21, na kikubwa kuliko chote ni kwamba simu janja ndiyo zinazidi kuongezeka katika soko kuliko simu za kawaida (Featured Phones).

mauzo ya simu

Ila kama unavyoona hapo juu soko la simu za kawaida linazidi kushuka, simu janja zinazidi kuitajika zaidi.

SOMA PIA:  Snapchat waanza kuuza Miwani za kurekodia video huko Marekani

2. Inakisiwa kufikia mwaka 2020  asilimia 80 ya watu wazima duniani kote watakuwa wanamiliki simu janja, tena iliyounganishwa na huduma za intaneti.

3. Kutoka kwenye idadi nzima ya watu bilioni 7.2 duniani kote;

 • Watu bilioni 4.2 hawana huduma ya intaneti
  Bilioni 3.6 hawamiliki simu
  Bilioni 5.1 hawapo kwenye mitandao ya kijamiii

B-AGhc9IQAAjcax

4.  Masoko ya Apps ya App Store kwa Apple na Google Play kwa simu za Android zina apps zaidi ya milioni 3. Apple kupitia  Appstore walikuwa na mapato ya zaidi ya Tsh Trilioni 25.8 kwa mwaka 2014 tuu!

5. Jumla ya simu bilioni 2 ziliuzwa kwa mwaka 2014! Na inategemewa mwaka huu zitauzika zaidi kwani bado soko linazidi kukua.

6. Nchi saba zinazoongeza kwa watumiaji wa intaneti duniani;

 • China – Milioni 641
 • Marekani – Milioni 280
 • India – Milioni 243
 • Japan – Milioni 109
 • Brazil – Milioni 108
 • Russia – Milioni 84
 • Germany – Milioni 71
SOMA PIA:  Maboresho: Instagram Direct yazidi kunogeshwa .

7. Asilimia 40 ya utumiaji wa intaneti duniani unashikiliwa na watu kutumia mitandao ya Facebook na YouTube.

Utumiaji wa Intaneti Duniani Kote

Utumiaji wa Intaneti Duniani Kote

Je ni data gani imekufurahisha sana katika hizi?

Endelea kusoma TeknoKona, kumbuka kusambaza maujanja na mahabari ya TeknoKona wengine pia wapate kufahamu! Ungana nasi pia kupitia  Twitter, Facebook na Instagram

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com