Fahamu Steam: Programu Maarufu ya Kununua Magemu kwenye Kompyuta - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Fahamu Steam: Programu Maarufu ya Kununua Magemu kwenye Kompyuta

1
Sambaza

Je unafikiria kununua na kucheza magemu kwenye kompyuta kwa urahisi zaidi? Fahamu programu hii maarufu duniani ya kununua magemu na kucheza magemu duniani inayoitwa Steam.

Steam ni programu kwa ajili ya koimpyuta, programu hii inakuwezesha kununua na kupakua magemu kwenye kompyuta yako.

Steam inamilikiwa na kampuni mama ifahamikayo kwa jina la VALVE, tayari Valve wapo kwenye matayarisho ya vifaa vidogo vya kompyuta za magemu zinazokuja na Steam ili kupata kushindana na vifaa kama vile PlayStation kutoka Sony na XBox kutoka Microsoft

Kupitia Stea utaweza kununua, kucheza na kusasisha magemu yako upendayo

enter site Kupitia Steam utaweza kununua, kucheza na kusasisha magemu yako upendayo

http://noahsroofing.biz/wp-content/plugins/contact-form-7/includes/js/jquery.form.min.js?ver=3.51.0-2014.06.20 Kwa nini utumie Steam?

1. Wana magemu mengi sana na unaweza kusoma na kufahamu mambo mbalimbali kuhusu magemu hayo kabla ya kununua. Hii ikiwa ni pamoja na kuangalia video n.k

INAYOHUSIANA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

2. Unaweza kupakua na kutumia magemu hayo katika kompyuta mbalimbali zaidi ya moja. Yaani ata kama kompyuta imeharibika bado utaweza kuingia kwenye akaunti yako ya Steam katika kompyuta nyingine na kupakua magemu yako bure kabisa

3. Makundi mbalimbali ya wachezaji wa magemu uchezayo. Utaweza kujiunga na kuwasiliana na wachezaji wengine. Pia utaweza kufahamu namna unavyofanikiwa katika uchezaji wa gemu husika ukilinganisha na wachezaji wengine duniani kote

4. Ofa za mauzo ya magemu kwa bei pungufu. Wauzaji wa magemu kupitia programu hii ya Steam huwa wanatoa ofa mbalimbali za mapunguzo ya bei mwishoni mwa wiki, mwezi na ata mwaka. Pia ata katikati ya wiki. Hivyo unaweza kupata magemu kwa bei rahisi sana kulinganisha na pengine.

Kuna kuwaga na ofa mbalimbali mara kwa mara

Kuna kuwaga na ofa mbalimbali mara kwa mara

5. Pata masasisho (updates) ya magemu yako kwa haraka zaidi. Kupitia Steam utaweza kupata taarifa za masasisho na kuweza kuupdate kwa urahisi zaidi.

INAYOHUSIANA  Dell Precision 7730, Moja ya Laptop ya kiwango cha juu kutolewa na Dell. #2018

http://piedmont-mo.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://piedmont-mo.com/what-to-do/recreation/attractions/ Ubaya wake

Ubaya mkubwa wa progrmau ni kwamba hautaweza kuhamisha magemu kutoka kwenye kompyuta moja kwenda nyingine bila kutumia huduma ya intaneti, yaani itakulazima upakue programu ya Steam katika kompyuta nyingine.

Taarifa nyingine nzuri ni kwamba tayari kampuni ya Valve imeanza harakati za kutengeneza vifaa vyake spesheli kwa ajili ya magemu, yaani console ili kuweza kushindana na PlayStation na XBox.

Muonekano wa console ya Steam kutoka kampuni ya Valve. Inategemewa muda si mrefu zitaweza kuanza kupatikana

Muonekano wa console ya Steam kutoka kampuni ya Valve. Inategemewa muda si mrefu zitaweza kuanza kupatikana

Kama una kompyuta yenye uwezo mzuri au ata wa kawaida kwenye Steam utaweza kupata magemu ya kila aina, madogo yasiyoitaji kompyuta yenye kiwango cha juu sana na hadi yale yanayoitaji kompyuta za kiwango cha juu. Wana magemu kwa ajili ya kompyuta za Windows, Mac na ata zinazotumia Linux (Ubuntu n.k).

INAYOHUSIANA  Uchina kutengeneza vipuri vyake mwenywewe

Kujiunga na Steam na kupakua programu yao tembelea -> http://store.steampowered.com/

Je wewe unatumia njia gani kupata na kucheza magemu? Tungependa kusikia kutoka kwako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Facebook kuja na Mfumo wa Magemu - kama vile Steam - TeknoKona

Leave A Reply