Fahamu Tofauti Kati ya Diski za SSD na HDD - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Fahamu Tofauti Kati ya Diski za SSD na HDD

0
Sambaza

Je ushawahi kukutana na diski za SSD? Umejua tofauti zake na zile zinazotumia HDD? Kama unampango wa kununua kompyuta au diski ya uhifadhi data basi ni muhimu ufahamu tofauti kati ya teknolojia hizi mbili – kwani kulingana na mahitaji yako ya kompyuta unatakiwa kufanya maamuzi sahihi..

HDD, kwa kilefu ni Hard Disk Drive wakati SSD ni Solid State Disk. Tofauti kubwa katika teknolojia hizi zipo kwa jinsi vifaa hivi vinavyotengeneza na jinsi vinavyohifadhi na kusoma data zilizohifaziwa ndani yake.

HDD ndiyo teknolojia ya muda mrefu zaidi wakati SDD ni teknolojia ya kisasa zaidi.

Diski za mfumo wa HDD unategemea mzungusho wa diski ya mviringo ndani yake inayohifadhi data unazoweka, na usomaji wa data hiyo huwa unafanyika wakati diski hiyo ikizunguka. Mfumo wa teknolojia ya SSD ni tofauti na huu, kwenye SDD data zinahifaziwa kwenye chip ndogo za kielektroniki na hivyo hakuna kitu kinachozunguka ndani yake. Diski ndogo za ‘USB Flash’ tunazotumia ni mfano mzuri wa teknolojia hii ya SSD.

Ukimya

Uwepo wa vitu vingi pamoja na suala la kuzungusha diski ndani yake HDD zinatoa sauti sana ukizilinganisha na SSD.

wakati HDD itatoa muungurumo wakati inatumika SDD itafanya kazi bila kutoa sauti yeyote

Ufanisi

HDD zinachukua muda mrefu zaidi katika kusoma na kuhamisha data wakati diski za mfumo wa SDD zinakuwa na kasi kubwa na hii ya yote ni kutokana na kutoitaji hatua nyingi katika usomaji wake wa data. Usomaji wa data katika diski ya SDD ni zaidi ya mara 60-100 haraka zaidi ukilinganisha na HDD. Hii inamaana kama ulikuwa unahamisha mafaili (copying) katika diski uhifadhi ya SDD mafaili hayo yatahamishika haraka zaidi ukilinganisha na kwenye HDD.

  • ‘Spidi ya kuhamisha mafaili katika SSD ni kati ya MB 200 – 500 kwa sekunde, wakati kwenye HDD ni kati ya MB 50 – 120 kwa sekunde kwenye kompyuta yenye sifa nzuri
  • Kwa wastani kompyuta inayotumia diski ya SSD kama Drive C itawaka haraka zaidi kwa zaidi ya mara 3 ukilinganisha na kompyuta inayotumia diski ya HDD kama Drive C.
Mlinganisho wa spidi ya ufunguaji wa programu kadhaa kati ya kompyuta inayotumia SSD na HDD

Mlinganisho wa spidi ya ufunguaji wa programu kadhaa kati ya kompyuta inayotumia SSD na HDD – muda ni katika sekunde

Programu kama magemu na nyingine nzito kama za kutengeneza video n.k zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi kwenye kompyuta inayotumia diski ya SSD kuliko kwenye HDD. Kwa mfano programu maarufu ya Adobe Photoshop inafanya kazi kwa haraka wa zaidi ya mara mbili kwenye kompyuta yenye diski ya SSD ukilinganisha na yenye HDD.

Kudumu kwa muda mrefu

Katika suala la kudumu pia ni diski za teknolojia ya SSD ndio zinaongoza, utafiti umeonesha kuna uwezekano wa asilimia 4 hadi 6 kwa diski ya HDD kuharibika ndani ya mwaka, wakati kwa diski ya SSD uwezekano wa kuharibika ni 1/10 ya asilimia 1. Huu ni uwezekano mdogo sana. (chanzo – networkworld.com)

Utofauti kwa ndani

Utofauti kwa ndani

HDD inamavitu mengi ndani ambavyo vinaweza haribika kwa urahisi pale mtikisiko wowote ukitokea ndani yake, mfano kompyuta ikiangushwa n.k

Utumiaji chaji (umeme)

Pia diski za SSD zinatumia umeme mdogo zaidi katika kufanya kazi, inasemekana katika kufanya kazi HDD itakapotumia Watts 6-7 diski ya SSD itatumia Watts 2-4, hii ni takribani nusu ya kiwango cha HDD. Inasemekana mtumiaji wa laptop yenye diski ya SSD atapata dakika 30 zaidi za chaji ukilinganisha na laptop yenye diski ya HDD. (chanzo – storagereview.com)

Uzito

Kutokana na kutokuwa na vitu vingi ndani diski za SSD ni nyepesi zaidi ukulinganisha na za HDD (ata kama ni za kiwango kimoja cha diski ujazo).ssd-vs-hdd-image

Ipi ni bora?

Ukiangalia kwa haraka ni kweli teknolojia ya diski za SSD ni bora zaidi lakini hii haimaanishi HDD haifai. Uamuzi utategemea vitu vingi.

http://forensor-project.eu/tag/testing/ Unaweza chagua kununua external diski au kompyuta yenye HDD kama;

  • Hutaki kutumia pesa nyingi, bajeti hairuhusu – hii ni kwa sababu diski ya ujazo sawa ya SSD itauzwa kwa bei ya juu zaidi ukilinganisha na bei ya ujazo huo huo kwa diski ya HDD
  • Hujali sana suala la uwezo wa kompyuta kuwa haraka zaidi katuka kufungua mafaili, kuhamisha n.k

http://touchlinevideo.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=https://touchlinevideo.com/2017-events/champcup17/ Kununua kompyuta yenye diski ya SSD itakufaa zaidi kama;

  • Unataka kutumia kompyuta husika kwa ajili ya uchezaji wa magemu au kutumia programu zinazoitaji kompyuta ya kasi zaidi mfano programu za Adobe n.k

source link Je ulikuwa unajiuliza kwa muda mrefu juu ya tofauti kati ya diski za SSD na HDD? Leo umezifahamu. Endelea kutembelea mtandao wako wa TeknoKona na kumbuka kusambaza makala kwa marafiki.

*picha - pcmag na mitandao mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply