Fairphone 2: Dondosha Simu Hii Kadri Unavyoweza! #Uchambuzi - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Fairphone 2: Dondosha Simu Hii Kadri Unavyoweza! #Uchambuzi

2
Sambaza

Simu janja zetu mara nyingi ni zile ambazo ziko kama mayai – ukiiangusha inabidi ufumbe macho, usali kisha ndio uiokote – kama imenusurika kuvunjika kioo hongera zako. Lakini vipi kama kioo kizima kimevunjika? Wakati baadhi ya watu wakiofia jambo hili kuna wengine hawana wasi wasi kabisa

enter
Kuna simu ambayo inatumia mfumo wa Android ambayo inaweza kukaa miaka na miaka na ikiweza kabisa kuhimili mikikimikiki na shuruba zingine zinazozikuta simu janja kama vile kuanguka.

fairphone_2

source url fairphone_2

Simu Hiyo inajulikana kama Fairphone 2, simu hii imetengenezwa kwa teknolojia ya aina yake ambayo inaweza himili karibia kila kitu

Simu Hii kwa ufupi iliandikwa kwenye makala ya: Simu 5 Za Ajabu Ambazo Ni Mbadala Wa Samsung Na Apple!

Pia kizuri katika simu hii ni kwamba inampa uwezo wa mtu wa kawaida kuweza kufungua bila ya kutumia kifaa chochote kwenye sehemu mbili ambazo ni rahisi sana kuharibika katika simu yoyote. Yaani katika skrini au betri, maeneo yote haya mawili mtumiaji anaweza akafungua na kurudishia vifaa (vipya) bila wasi wasi

Muonekano Wa FairPhone 2 Ikifunguliwa

Muonekano Wa FairPhone 2 Ikifunguliwa

http://pncwinterfest.com/about/promotions/ Fairphone wenyewe wanasema kuwa wana imani kwa kupitia simu yao basi wateja wao watakuwa na mahusiano mazuri sana na simu zao. Je wewe una mahusino mazuri na simu yako sasa?

INAYOHUSIANA  Apple wameboresha/kuleta vitu vipya kwenye iOS 12

Kama unayo bila shaka utakuwa umeshaangalia kama simu yako ni feki au la

Rangi Za Simu Hiyo

Rangi Za Simu Hiyo

Simu hii ni ya ajabu kidogo sio? Ukilinganisha na zile simu janja tulizo zizoea sana. Usishangae lakini maana teknolojia inakuwa kwa kiasi kikubwa sana siku hizi. Kwa karne hii lolote linawezekana kupitia teknolojia

Niandikie sehemu ya comment hapo chini ukinielezea lako la moyoni kuhusu mapokezi yako juu ya simu hii. Pia kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com