FBI iliwalipa wadukuzi kufungua iPhone ya Magaidi nchini Marekani

0
Sambaza

Vyanzo vya habari vinasema kwamba FBI waliifungua simu ya magaidi waliotekeleza shambulio la San Bernadino kwa msaada wa wadukuzi ambao waligundua udhaifu ambao upo katika simu hiyo na kuutumia kuifungua bila kufuta data.

Kama hujui chochote kuhusu ugomvi wa Apple na FBI, kwa ufupi ni kwamba….

Disemba mbili mwaka 2015 kulitokea shambulio la kigaidi California ambalo lilihusisha wanandoa wawili ambao waliwaua watu 14 kwa kuwafyatulia risasi na kuwajeruhi watu 22. Polisi iliwatafuta na kuwaua magaidi hawa masaa kadhaa baada ya tukio hilo, katika vitu ambavyo polisi walivipata baada ya msako ilikuwa ni simu moja ya iPhone ambayo ilikuwa imefungwa kwa password.

Apple walipoombwa waifungue simu hiyo walikataa kwa madai kwamba swala hilo linapingana na sheria zao za usiri, hii ilipelekea FBI na Apple kupelekana mahakamani ili kupata suluhu lakini swala likiwa mahakamani FBI wameweza kuifungua simu hiyo kwa msaada wa wadukuzi na makala hii inaangalia jinsi wadukuzi hao walivyoweza kuifungua simu hiyo.

FBI

Magaidi waliotekeleza shambulio la San Bernadino

la-me-ln-fbi-apple-san-bernardino-phone-20160216

Wadukuzi hao watakuwa wamelipwa pesa nyingi baada ya kuchunguza na kupata kosa la kiprogramu la Apple katika simu hiyo ya iPhone ambalo linaweza kutumiwa kuingia katika simu bila ya kufuta data ambazo zilikuwapo katika simu hiyo.

Baada ya kupata kosa hilo la kiprogramu katika simu hiyo wadukuzi hao kwa kushirikiana na FBI walitengeneza programu nyingine ambayo iliondoa uwezo wa simu hiyo kufuta data zote ambazo zilikuwa katika simu hiyo kipindi pale password ya simu hiyo ikiondolewa na programu yao.

Hii ina maana moja tu kwa watumiaji wa simu za iPhone kwamba kwa kiasi fulani simu hizi ambazo zinatajwa kuwa salama zaidi bado sio salama kama tulivyodhani, ingawa FBI wamesema njia waliyotumia kufungua simu hiyo haifanyi kazi kwa kila simu lakini bado safari ipo kupata simu ambayo ni salama kwa asilimia mia.

SOMA PIA:  Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiiana! #Teknolojia

FBI

Kwa upande mwingine Wadukuzi hawa wamewapa moyo vijana wa Afrika mashariki ambao kwa namna moja au nyingine wanataka kuwa wadukuzi wema siku za usoni kwani wameonesha kwamba udukuzi wenye nia ya kuboresha usalama wa taifa bado unahitajika na bado unatumika.

Vyanzo: The Washington Post na mitandao mingine.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com