Gemu la FIFA 18: Toleo la bure kabisa lapatikana ndani ya siku 1

Gemu la FIFA 18: Toleo la bure kabisa lapatikana ndani ya siku 1

0
Sambaza

Kampuni ya EA Sports, watengenezaji wa magemu maarufu ikiwa ni pamoja na magemu yanayotoka kila mwaka ya mchezo wa mpira wa miguu yanayobeba jina la FIFA wapo katika wakati mgumu baada ya wadukuzi kuweza kuwashinda maujanja.

http://ammofightleague.com/ammo-fl-logo/ Toleo jipya la gemu la FIFA 18 lilianza kupatikana rasmi tarehe 29 mwezi wa tisa na ndani ya masaa 24 wadukuzi walifanikiwa kushinda hatua za kiusalama za ndani ya gemu hilo na kuwezesha upatikanaji wa toleo la gemu hilo bure kabisa kwa maelfu ya watu kupitia mfumo wa Torrents.

Fincar prescription online next day delivery Baada ya udukuzi huu ina maana mtu yeyote mwenye kompyuta anaweza kushusha/download na kupakua/install toleo la gemu hilo kwenye kompyuta yake bila malipo yeyote.

Nini kilitokea hadi toleo la gemu la FIFA 18 kuweza kuchezewa kiurahisi namna hii kiteknolojia?

Inasemekana kikubwa ni kwamba kampuni hiyo ilibadili teknolojia inayotumia kiulinzi dhidi ya utumiaji wa gemu hilo bila malipo. Kampuni mpya iliyotoa teknolojia ya usalama dhidi ya udanganyifu huo ya Denuvo Technologies imejiweka katika nafasi mbaya kibiashara baada ya tukio hili.

INAYOHUSIANA  Kodi kwenye mitandao ya kijamii yaanza rasmi Uganda

Hii inamaanisha hakuna kampuni nyingine kubwa itaamini kutumia teknolojia ya usalama kutoka Denuvo kwa ajili ya kulinda bidhaa zake dhidi ya udukuzi unaoweza kusababisha kukosekana kwa mapato.

Toleo la FIFA 18 lilikuwa ni moja la toleo la gemu lililokuwa linasubiriwa kwa hamu sana na wacheza magemu ya mpira na inasemekana mapato yake yatakuwa chini ukilinganisha na kama gemu hilo lisingeweza kupatikana kwa njia ya udanganyifu.

fifa 18 steampunks

go Ila wanaodownload gemu hilo wajikuta na uhitaji wa zaidi ya GB 30

Kikundi cha wadukuzi maarufu wa Steampunks ndio kilichohusika na kuwezesha uwezo wa gemu hili maarufu kutumika bure kabisa bila malipo.

Tayari EA Sports wameondoa teknolojia ya Denuvo kwenye baadhi ya magemu yao yanayokuja. Kwa FIFA 18 hakuna tena kinachoweza kufanyika kwa EA Sports, mabadiliko pekee ni hadi tena toleo la FIFA 19 litakapokuja.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.