FIFA: Teknolojia ya video kutumika kombe la Dunia 2018 Urusi - TeknoKona Teknolojia Tanzania

FIFA: Teknolojia ya video kutumika kombe la Dunia 2018 Urusi

0
Sambaza

Shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA limeruhusu rasmi matumizi ya teknolojia ya video yaani Video Assistant Refrees (VAR) kutumika katika mechi za Kombe la Dunia 2018 mwezi Juni huko nchini Urusi.

Finpecia 1mg tablets VAR itasaidia kufanya maamuzi ambayo yametolewa na mwamuzi wa uwanjani lakini hayakuwa sahihi na hii itasaidia kupunguza nafasi ya nchi nyingi kurudi nyumbani mapema kutokana na maamuzi yenye makosa.

Teknolojia ya video

http://icareforchildren.org/what-we-do-3__trashed/nf-december-6-march-7-2018/ Video Assistant Referee (VAR) ikionekana katika uwanja wa John Smith, Huddersfield, katika mashindano ya Emirates FA Cup, raundi ya tano.

see Kupitishwa kwa teknolojia ya VAR katika kombe la Dunia la mwaka huu kunaweza kuathiri nchi nyingi kuanza kutumia teknolojia hiyo katika ligi zao. Tayari ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga imeanza kutumia pamoja na ligi kuu ya Uhispania, La Liga imeahidi kutumia msimu ujao wa ligi kuu yao.

Teknolojia ya VAR itatumika pale ambapo mwamuzi wa ndani ya uwanja anapopatwa na utata wa alichokiamua, aidha kwa kutoa penati, kumpa mchezaji kadi asiyehusika, mchezaji kujiangusha, kama mpira umevuka goli, mchezaji ameotea au la pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza kuwa na uamuzi wenye utata.

Teknolojia ya video

Mwamuzi akipata msaada kutoka kwenye teknolojia ya VAR

Katika hali kama hizo mwamuzi ataruhusiwa kusimamisha mpira na atakwenda kulipokuwa na VAR ataangalia na kujiridhisha kama ni sahihi alichoamua au si sahihi. Mfano kama alikataa goli na teknoojia ya VAR ikaonesha ni goli sahihi basi atabadili maamuzi na kuhesabika ni goli sahihi.

Teknolojia ya video

Refa akipata usahihi wa kilichotokea uwanjani kupitia teknolojia ya VAR.

Matumizi ya teknolojia ya VAR yamekuwa ‘Yakililiwa’ kwa muda mrefu sana hasa mwaka 2010 wakati wa kombe la dunia lilipofanyika Afrika ya Kusini katika mechi baina ya Ujerumani na Uingereza mwamuzi alipokataa goli la halali la Frank Lampard kwa kuona mpira haukuvuka mstari wa goli ilihali ulivuka mstari.

INAYOHUSIANA  Msichana anusurika kifo kwa sababu ya 'Selfie'

Pamoja na ubora wa teknolojia ya VAR lakini washabiki wengi wa soka wanaona kama teknolojia hiyo itaondoa ladha ya mchezo huo kwa kusimama mara kwa mara kusubiri maamuzi ya VAR. Nini maoni yako kuhusu teknolojia ya VAR?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.