Flippy: Roboti mahususi kwa ajili ya upishi wa ‘Burger’! #Teknolojia

2
Sambaza

Imekuwa si kitu cha kushangaza tena kwa kusikia kuwa roboti anafanya kazi ambao hapo awali ilikuwa ni binadamu peke yake ndiye alikuwa akizifanya; hivi sasa wapishi wengi wanaweza kukosa kazi kwa wenzetu waliopo dunia ya kwanza.

Roboti mmoja maarufu kama “Flippy”  ametengenezwa kwa ajili ya migahawa, ni mtayarishaji wa kile chakula ambacho hakichukui muda mrefu kukitayarisha na kinapendwa na wengi, hapa namaanisha “Burger”.

Flippy hachukui muda mrefu kumuweka sawa ili aweze kuanza kufanya kazi zake. Inachukua muda wa takribani dakika 5 kuweza kumuweka Flippy sawa ili aweze kufanya kazi zake.

SOMA PIA:  PowerShake: Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi #Maujanja

flippy

Miso Robotics, ambao ndio waliomtengeneza roboti Flippy wamesema wameanza na upishi wa burger ambalo si pishi gumu ila huo ni mwanzo tu na matarajio yao ni kwa roboti kuweza kujua mapishi mbalimbali kupitia kwa wapishi wasaidizi (binadamu). Tazama vionjo ya roboti Flippy.

Flippy: Mkono wa kiroboti ukifanya kazi

flippy

Mgahawa wa CaliBurgers ambao ndio umekuwa wa kwanza katika matumizi ya roboti katika mapishi ya burger umesema kuwa mipango yake ni kuwa na roboti takribani hamsini katika migahawa yake iliyopo karibu dunia nzima.

Vyanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com