Simu ya Freedom 251 – Simu janja ya bei rahisi zaidi, Kuanza kupatikana Juni 30

1
Sambaza

Tulishawahi andika kuhusu ujio wa simu ya Freedom 251, simu ya bei rahisi zaidi duniani. Baada ya kusubiria kwa kipindi flani, tayari simu janja hiyo ipo tayari na itaanza kuuzika Juni 30 mwaka huu.

simu ya bei rahisi

Simu ya Freedom 251 itauzika kwa bei ya takribani Tsh 8,000/= | Ksh 410 (Dola 4 za Marekani), na hivyo kuchukua rekodi ya kuwa simu janja ya bei rahisi zaidi duniani.

Freedom 251 imetengenezwa na nani?

Simu janja hii ya Freedom 251 imetengenezwa na kampuni mpya tuu isiyo na ata miaka miwili katika biashara ya utengenezaji na uuzaji wa simu – Ringing Bells iliyopo katika jimbo la Uttar Pradesh huko nchini India.

SOMA PIA:  Hukumu ya Mahakama: Simu ya mkononi imesababisha uvimbe katika ubongo wa mtumiaji

Kampuni hiyo ya Ringing Bells imesema tayari ina simu 200,000 za Freedom 251 zikiwa tayari kuingia sokoni, hayo yalisemwa na mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Mohit Goel.

freedom-251-simu

Ina sifa gani?

  • Inakuja na toleo la Android 5.1 Lollipop
  • Kamera ya selfie ya megapixel 0.3 na ile kuu ikiwa ni ya megapixel 3.2
  • Inakubali teknolojia za 2G na 3G pamoja na WiFi
  • Ina betri la mAh 1450
  • Kioo (display) cha sentimita 10
  • Prosesa ya 1.3GHz quad-core
  • RAM ya GB 1 pamoja na diski uhifadhi (storage) wa GB 8 – unaweza kutumia memori kadi (SD Card) ya hadi GB 32

Pia inakuja na apps muhimu kama vile Google Play, WhatsApp, Facebook, YouTube na zingine muhimu kwa watumiaji wa nchini India.

Je wanatengeneza faida?

Mkurugenzi wa Ringing Bells amesema kwa sasa hawatengenezi faida katika simu hizi ila wanategemea kupata faida kama watafanikiwa kuuza simu hizo kwa wingi zaidi.

SOMA PIA:  Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

Inasemekana soko lipo kinachotakiwa kwa simu hizo ni ubora tuu na kama watafanikiwa huko nchini India basi inawezekana kabisa simu hizo zikafika hadi katika mataifa mengine hasa Afrika na huko Asia.

Je una mtazamo gani juu ya simu hii? Tuambie kwenye comment

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com