Fuchsia OS: Google wanatengeneza Programu Endeshaji (OS) nyingine!

Fuchsia OS: Google wanatengeneza Programu Endeshaji (OS) nyingine!

0
Sambaza

Google wanakuja na programu endeshaji nyingine nje ya Android na Chrome OS. Programu endeshaji hiyo inayokwenda kwa jina la Fuchsia tofauti na Android na Chrome OS hii inajitegemea na haitatumia Linux.

go to link

get link Google Fuchsia OS

Fuchsia ni ya nini?

buy cipla Finax Inasemekana programu endeshaji ya Fuchsia inalenga zaidi kutumika katika vifaa vingine vya kisasa kama vile friji, mifumo ya usalama, n.k na si kushindana na Android na Chrome OS kwenye simu na laptop.

Android na Chrome OS zinazotengenezwa na Google zitaendelea kuwepo ila wameona ni muhimu kuwa na programu endeshaji nyingine nyepesi kwa ajili ya kutumika kwenye vifaa janja vya kisasa.

Inaonekana Google wanachukua hatua kama zilizochukuliwa na Samsung, ambapo Samsung wanamiliki programu endeshaji ya Tinzen OS ambayo wanaitumia kwenye vifaa janja ambavyo wanaona hakuna ulazima wa kutumia Android nzima.

Android OS inazidi kukua na ukuaji wake unaifanya isifae sana kutumika katika vifaa nje ya Simu, Tableti, kompyuta n.k.

Vyanzo: AndroidPolice na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.