Julian: Fundi simu milionea aliyejifunza ufundi mtandaoni

0
Sambaza

Sehemu kubwa ya maisha yetu kwa sasa yanategemea sana mawasiliano ya kimtandao. Fursa nyingi zimekuwa zikipatikana pia kwa njia ya mitandao.

Kwenye mitandao kwa sasa kuna kila kitu kuanzia mawaidha ya dini, kujifunza namna ya kupika, namna ya kuvaa, namna ya utengezaji wa vitu mbalimbali. Kuna fursa pana ni kiasi tu cha kujiongeza.

Mmoja wa watu waliotumia vizuri fursa zinazopatikana kupitia mitandao ni kijana mdogo anayejulikana kwa jina la Julian Shovlin. Kwa sasa ni fundi Tajiri na mahiri katika kutengeneza simu za aina mbalimbali.

Juliana hakusomea kazi ya kutengeneza simu bali alijifunza kupitia mitandao kadhaa inayoelezea namna ya kutengeneza na kurekebisha simu.

Ilikuwaje akawa fundi simu, nini kilimpelekea kujifunza utengenezaji wa simu?

Kisa hasa cha kijana huyo mwenye busara Julian Shovlin ni pale alipopatwa na mfadhaiko kwa kudondokewa na simu yake mpya kwa mara ya pili.

fundi simu milionea

fundi simu milionea: Julian Shovlin

Kudondoka huko kulipelekea simu yake kukatika kioo na hapo ndipo aliamua kujaribu na kuirekebisha mwenyewe.

SOMA PIA:  Google yaruhusu mtu kuweza kutengeneza "Google Maps" zake na kuzisambaza

Aliamua kuangalia mafunzo kadhaa ya video kwenye mtandao na akajifunza mwenyewe jinsi ya kufanya hivyo.

Ulikuwa uamuzi mzuri! Julian alitambua kwamba alikuwa hawezi kumudu gharama ya simu mpya kwani wakati huo alikuwa mwaka wa pili wa chuo kikuu.

Akiwa mwaka wa pili chuo ndipo alianzisha biashara ya kurekebisha simu. Julian alifungua duka lake la kwanza huko London mwezi Agosti 2013.

Julian anasema, “Nilijitengenezea nafasi hii baada ya kuidondosha simu yangu mara kadhaa na kuvunjika kioo chake. Baada ya kuwa na uzoefu wa kurekebisha kioo, niliamua kununua vifaa vya matengenezo na kujifunza mwenyewe kupitia video za mafunzo mtandaoni.”

Anaongeza kusema, “Niligundua kuna haja na uhitaji halisi wa fundi simu. Mwanzo Ilikuwa ni kwa ajili ya familia na marafiki tu, kisha nikaanzisha ukurasa wa Facebook na kuanza kuchukua kazi kupitia mtandaoni.”

Anaelezea, “Sikujua mengi juu ya masoko lakini mara moja watu walikuwa wakiingia. Nadhani hii  ilikuwa kwa sababu kabla ya hapo hawakujua wapi panapatikana huduma ya kutengeza simu zao kwa haraka. Kulikuwa na maduka machache ambayo hayakujitambulisha rasmi yaliyokuwa yakitoa huduma kama yangu.”

fundi simu milionea

Fundi Simu Milionea: Muonekano wa moja ya maduka yake ya iSmash

Kampuni hiyo sasa imefanikiwa sana na kwa mwaka huu tu ameingiza paundi milioni 13 akiwa na umri wa miaka 26 tu.

SOMA PIA:  Instagram yazidi kuiiga Snapchat, yaleta face filters na Hashtags

Amefungua duka lake la 17 la kurekebisha simu katikati ya jiji la Manchester eneo linalofahamika kama Arndale. Maduka yake yanafahamika kwa jina la iSmash.

Duka lake la Manchester ni la kwanza kaskazini ya Uingereza. Julian anasema sababu ya kufungua duka katika mji huo ni kwamba, “Tulichagua Arndale kwa sababu ina muingiliano mwingi wa watu na biashara na Kuna ushindani mdogo sana katika soko la utengenezaji wa simu.”

Sasa anaangalia maeneo mengine katika jiji hilo kama ya Kituo cha Trafford na kituo cha treni cha Piccadilly.

SOMA PIA:  Cubimorph: Fikiria kuwa na simu yenye uwezo wa kukunjwa na kupangwa vile upendavyo

Mafundi katika maduka yake wanaweza kurekebisha skrini zilizovunjika katika Simu Janja, Laptop, Tablet na matatizo kadhaa yanayojitokeza katika vifaa hivyo.

Kinachovutia wateja ni uharaka wa utengenezaji. Muda wa kutengeneza ni wastani wa dakika 30. Kuhusiana na hilo anasema, “Watu hawataki kuwa bila simu zao kwa masaa kadhaa, ni vizuri kuharakisha.”

Julian, ambaye anatoka mji wa Dublin amesomea kozi ya biashara na uchumi katika Chuo cha Trinity,analenga kuwa na maduka 25 mwishoni mwa mwaka huu na maduka 50 katikati ya mwaka 2019.

Ni kisa kizuri na cha kweli cha kijana aliyeweza kutumia fursa vizuri. Je una maoni gani kuhusu makala haya? tuandikie hapo chini sehemu ya maoni ili wengine wanufaike katika maoni yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com