Ni wazi kuwa simu mbili ambazo zinatarajiwa kutambulishwa katika mwezi oktoba ni mwendelezo wa matoleo ya Pixel.. Yaani Pixel 2 na Pixel 2 XL.
Mpaka sasa wengi wameshapata fununu juu ya sifa ambazo simu hizo mbili (Pixel 2 Na Pixel 2 XL)zitakuja nazo lakini cha kushangaza ni kwamba kwa sasa zimeibuka taarifa zingine (fununu) ambazo zinasema kuwa zitatoka simu tatu na sio mbili kama ilivyokua inategemea mara ya kwanza
Simu ya Tatu itajulikana kama ‘Ultra Pixel’ na itakuja na fununu zinasema kuwa itakuja ikiwa na kamera mbili.
Kumbuka kitu kama hichi cha kuachia simu tatu kwa mkupuo kimefanyika na makampuni mengi ya simu na hata mwezi uliopita. .kampuni ya Apple iliachia simu tatu ambazo ni iPhone 8, iPhone 8 Plus na iPhone X.
Sifa nyingi za simu janja ya Ultra Pixel hazipo wazi..lakini fununu zinasema kuna uwezo wa alama za vidole katika uso wa skrini (display fingerprint). Vile vile kuna kitu kipya kinachoitwa ‘Fluid’ ambacho kinafanya kazi sawa na iPhone X katika swala zima la kuhisi (Gesture) kwa sababu haina kitufe cha ‘Home’
Angalia Video Kujua Sifa Hizo (Fununu)
Hii ni fununu tuu ..simu inaweza ikawepo au siwepo na vile vile inaweza ikawepo ila isiwe na sifa hizi ikawa na sifa zingine kabisa. Cha msingi ni tusubirie tuu matoleo hayo yakitoka au taarifa kamili kutoka vyanzo vinavyoaminika.