Fununu Kuhusu Samsung Galaxy Note 6!

0
Sambaza

Kampuni la Samsung lipo mbioni kuja na simu janja ya Note 6. Simu hii bado haijatoka lakini vyanzo mbali mbali vimeandika kuhusu fununu za ujio huo. Leo teknokona imekuandalia fununu hiyo kwa ufupi

Kampuni la Samsung lina mafanikio makubwa sana na mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yametokana na mauzo ya simu zake

Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kampuni kwa kupitia matoleo yao ya ‘Note’ Samsung wameona wasilale na kuendelea kutoa matoleo ya simu hizi ikiwa yana maboresho mengi zaidi kulingana na soko.

Samsung Galaxy

Samsung Galaxy  Note

Kwa sasa kampuni inategemewa kuja (kutoa) toleo lake la Note 6 kwani kwa sasa Note 5 iko tayari sokoni. Simu hii bado haijatoka na kuna fununu kadha wa kadha juu yake.

SOMA PIA:  Jiandallae 3: Simu Janja mpya kutoka Korea Kaskazini

Simu hii inategemewa kuwa na ukubwa wa kioo cha inchi 5.8 na itakuwa na GB 6 za ukubwa wa RAM. Licha ya kuwa Note 5 haikufanya vizuri sana mwaka jana (ilipo achiwa) hili bado halijawakatisha tamaa Samsung. Bado wanapambana kuhakikisha bado wanamiliki soko lao kwa kufanya maboresho zaidi.

Lakini kama ukiniuliza mimi kwanini mauzo ya Note 5 yalifanya vibaya ntakuambia sababu ni kwamba walitoa simu mbili kali sana za mwendelezo wa Galaxy S ( S6 na S6 Edge). Hili ni moja kati ya mambo ambayo yalipunguza mauzo ya simu hizo kwani matoleo hayo mawili yalishika soko sana.

SOMA PIA:  Hii ndio simu ya Nokia 3310 katika upya wake mwaka 2017!

Lakini kwa mteja ambaye anapenda simu za Samsung za mfumo ule wa Note humwambii kitu kutokana na simu hizi.

Sehemu Ya Nyuma Ya Simu Ya Note

Sehemu Ya Nyuma Ya Simu Ya Note

Fununu ni kwamba simu hizo zitatokwa kwa matoleo ya aina tatu; Standard, Edge na nyingine katika mfumo wa kukunja. Fununu hizi zimetoka katika vianzo mbali mbali hivyo zinaweza kuwa ni fununu tuu

Note 6 inasemekana kuwa itakuwa na betri la uwezo wa mAh 4500 na pia itakuwa na wembamba mkubwa tuu. Na vile vile inategemewa kwa kiasi kikiubwa kuja na programu endeshaji (OS) mpya ya Android N.

SOMA PIA:  Mwanzilishi Wa Android Anakuja Na Simu Yake, Mei 2017! #Muendelezo

MUHIMU: Samsung bado wao hawajatoa taarifa kamili kuhusiana na ujio wa simu hii hivyo usije ukashangaa kuwa hakutakuwa na simu kama hiyo kutoka Samsung au ikatoka sema ikawa na sifa tofauti kama hizi tolizoandika.

Tupia lako la moyoni hapo chini sehemu ya comment. Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali ya kiteknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com