FUNUNU: Twitter Iko Sokoni Na Makampuni Haya Ndiyo Yanaitolea Macho!

0
Sambaza

Twitter ni moja kati ya mitandao ya kijamii mikubwa kabisa, ukiachana na ukubwa na thamani yake lakini kampuni hiyo imekuwa ikipata shida kutengeneza faida ya kibiashara kupitia huduma zake.


Twitter imekua ikipata faida ndogo – ile ambayo hawakuitegemea – kwa kipindi cha muda mrefu. Fununu ni kwamba kampuni iko sokoni, kulingana na thamani yake pengengine inaweza ikanunuliwa na makampuni haya.

1. Salesforce
2. Google
3. Microsoft
4. Verizon

airtel tanzania bando

twitter

Vyanzo mbalimbali vinasema kuwa maongezi mengi yanatokea katika upande wa Google/Alphabet na Salesforce.

Alphabet, kampuni ambayo inaimiliki kampuni ya Google ilikataa kutia neno katika habari hii. Salesforce na wenyewe walifunga midomo yao, Verizon ndio kampuni lingine ambalo liliongelewa katika ripoti mbalimbali kama mmoja kati ya yale ambayo yanaweza kununa kampuni ya Twitter.

SOMA PIA:  Instagram kuja na app kwa ajili ya kuchati tu

Kumbuka Hivi karibuni tuu Microsoft iliinunua LinkedIn na pia Verizon ipo kwenye hatua za mwisho za kununua Yahoo. Bila ya kusahau kuwa Google na Salesforce kuwa ni makampuni makubwa sana kwenye mambo ya teknolojia, sasa nani atawaweza kununua kampuni ya Twitter?

Twitter inakubali kujiuza lakini imesema haitajiuza kwa bei rahisi kama watu wengi wanavyidhani. Pengine wengi wameona kuwa haifanyi vizuri na wamedhani kuwa thamani yake ni ndogo.

Ripoti zimesema kuwa Twitter inafikiria kujiuza kwa thamani ya dola bilioni 30 za kimarekani kama ikiingia sokoni kwani kwa sasa inafanya maongezi tuu na makampuni hayo.

SOMA PIA:  Instagram yaleta uwezo wa kufuatilia Hashtag

Pengine inaweza ikaonekana kuwa hakuna presha kubwa inayotumika katika jambo hili, kutoka Twitter au katika hayo makampuni mengine. Hii isikishtue kwani mara nyingi ndivyo haya mambo yanavyooanza, si unakumbuka hata ishu ya Yahoo ilianza kama utani tuu?

Twitter inajivunia sifa kubwa kutokana na uwezo wake wa matangazo, video za simu, habari za punde na bila ya kusahau taarifa nyingi ambazo wanazo. Vitu vyote hivi vinaweza vikatumika na kampuni na vikaleta faida kubwa sana.

Vyanzo vingi vinasema Google ndio wanaweza wakalinunua kampuni hili kwa haraka zaidi bila ya kujifikiria sana kwani wana hela ya kutosha – kwa robo ya mwaka iliyopita Alphabeti iliingiza mapato ya dola bilioni 21 za kimarekani – tuu.

SOMA PIA:  Yahoo: Taarifa za akaunti bilioni 1 zadukuliwa

Tusubirie tuone nani atakuwa mshindi wa kuinyakua Twitter au kama kuna mambo yatabadilika? Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe unahisi nani atakuwa mstari wa mbele na kuweza kulinunua hili kampuni (Twitter). Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona kila siku ili kuwa karibu na maujanja na habari mbali mbali zinazohusu teknolojia. Ungana nasi pia kupitia Twitter @teknokona, Instagram @teknokona pamoja na Facebook @teknokona.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com