Galaxy Note Fan Edition: Samsung yatumia sehemu ya Note 7 kuunda simu mpya - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Galaxy Note Fan Edition: Samsung yatumia sehemu ya Note 7 kuunda simu mpya

0
Sambaza

Kampuni ya mawasiliano ya Samsung imeanza kuuza simu nyingine ambazo inasema imetumia baadhi ya sehemu na vipande vilivyokuwa kwenye simu za Galaxy Note 7 ambazo zilikumbwa na matatizo.

Keppra purchase canada

enter site Simu hizo za Galaxy Note 7 zilikuwa zinashika moto na kulipuka kutokana na tatizo kwenye betri zake.

http://muldavinlawfirmtn.com/drug-defense/ Kampuni hiyo imesema simu hizo mpya kwa Kiingereza Galaxy Note Fan Edition zitapunguza athari za kimazingira kutoka kwa mabaki ya simu hizo ambazo ziliacha kuuzwa kutokana na hitilafu hizo.

Simu hizo mpya zitauzwa Korea Kusini pekee na zitaanza kuuzwa tarehe 7 Julai.

Kampuni hiyo imesema simu hizo zitakuwa na betri ndogo ambazo ni salama zaidi kuliko simu hizo za awali.

Galaxy Note Fan Edition

Muonekano wa simu ya Note 7 kabla ya msukosuko wa matatizo ya betri

Samsung iliacha kuunda simu za Galaxy Note 7, ambayo ilifaa kuisaidia kampuni hiyo kushindana na simu mpya za iPhone, mwishoni mwa mwaka jana baada ya kwanza kuwaomba wateja wazirejeshe nzifanyiwe ukarabati lakini hatua hiyo ikakosa kufaulu.

INAYOHUSIANA  Samsung J2 Core ndio ya kwanza kuwa na Android Go

Inakadiriwa kwamba simu 2.5 milioni zilirejeshwa kwa kampuni hiyo.

Simu hiyo mpya itakwua na vipande kutoka kwa simu ambazo zilirejeshwa na wateja na vipande vingine kutoka kwa simu za Samsung ambazo hazikuwa zimeuzwa.

Samsung Galaxy Note Fan Edition

Muonekano wa simu ya Samsung Galaxy Note Fan Edition

Betri ndogo na bei nafuu

Watetezi wa mazingira wamekuwa wakiishinikiza Samsung kutumia tena baadhi ya sehemu za Galaxy Note 7 ili kupunguza taka ambazo zingetokana na simu hizo.

Inakadiriwa kwamba simu 400,000 mpya zitaanza kuuzwa kuanzia Ijumaa.

  • Bei yake itakuwa ni won 700,000 za Korea ($615; £472), ambayo ni 30% chini ya bei iliyokuwa ya Galaxy Note 7. Hii ni takribani Tsh 1,300,000/=.
  • Simu hizo zitakuwa na betri za 3,200 mAh na Samsung wanasema betri hizo zimechunguzwa vyema.
  • Note 7 zilitumia betri za nguvu ya 3,500 mAh.
INAYOHUSIANA  Hili ndio toleo la Nokia 7

Simu za Samsung Galaxy Note 8, ambazo zitatolewa kuifuata Note 7, zinatarajiwa kuanza kuuzwa baadaye mwaka huu.

Ingawa simu ya Samsung Galaxy Note Fan Edition imetolewa kwa soko la Korea tuu kwa sasa wengi wanaamini haitakuwa muda mrefu simu hizo kuanza kusambaa katika mataifa mengine kupitia wauzaji binafsi.

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.