Gari linaloweza kupaa kama ndege, suluhisho la muda kwa mahali unapoenda

0

Muda ni kitu ambacho hakiwezi kuthaminishwa na ni muhimu sana hivyo kila sekunde ina umuhimu wake katika maisha na kufika mahali kwa wakati ni jambo ambalo wengi (hasa kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea) wanathamini sana muda.

Foleni barabarani zimekuwa kero sana na hivyo kufanya watu kuchukia usafiri hasa kwa nchi zenye idadi kubwa ya usafiri binafsi barabarani. Kwa namna moja au nyinggine ndio maana wataalamu wa masuala ya teknolojia na wahandisi wakaamua kutengeneza gari linalopaa kama ndege! kuondoa adha ya mtu kukaa kwenye foleni.

Sifa za PAL-V Liberty (Gari lenye uwezo wa kupaa)

PAL-V limetengenezwa nchini Uholanzi likiwa na matairi matatu propela 2 na uwezo wa kubeba watu wawili. Likiwa linapaa matairi yake yanashuka kidogo chini yofauti na ndege zingine.

Kasi: Lina kasi ya Km 160/saa likiwa kama gari na kuweza kufika Km 100/saa ndani ya sekunde 9. Injini yake ina nguvu kiasi cha 100hp na kwenda umbali wa Km 1,315 kwa lita 100 za mafuta. Huku ikiwa kama ndege ina kasi ya Km 180/saa huku nguvu ya injini ikiwa 200hp.

Mwendo wa kawaida ni Km 140/saa na kutembea umbali wa Km 400 kwa ujazo wa mara moja wa tenki na kuweza kutembea umbali wa Km 500 iwapo mtu mmoja ndio anaiongoza. Ili kuweza kupaa inahitaji umbali wa mita 330 na umbali wa mita 15 kati yake na kitu chocohote mbele yake.

PAL-V Liberty ikiwa katika majaribio

Uzito: Ina uzito wa Kg 664 (bila abiria) na uwezo wa kupaa kwa uzito wa juu kabisa wa Kg 910. Lina uwezo wa kubeba mzigo wa mpaka Kg 20.

Mafuta: Haihitaji mafuta maalum ya ndege na hivyo unaweza kujaza mafuta katika sheli yoyote kulingana na aina ya mafuta ambayo injini yake inatumia.

Bei: PAL-V Liberty inauzwa kwa kuanzia bei ya $400,000| zaidi ya Tsh. Milioni 890.

PAL-V Liberty inategemewa kuanza kuuzwa mwakani na ili mtu aweze kuendesha anatakiwa awe pia na leseni ya urubani.

Vyanzo: GT Spirit, BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com