Sehemu mbalimbali duniani kucheza magemu ni sehemu mojawapo ya maisha na kwa wengine unafikia wakati anapata uraibu, sasa Google wapo mbioni kufanya majaribio gemu la Assassin’s Creed kwenye Chrome.
Tukizungumzia suala zima la magemu basi ni kawaida mtu kuzungumzia kompyuta/kifaa kingine maalum ambacho kimetengenezwa kwa ajili ya burudani hiyo. Google wanataka kujaribu kuambatanisha gemu la Assassin’s Creed kwenye kivinjari chake.
Badala ya kuwa na gemu hilo likiwa limehifadhiwa kwenye kompyuta, utaweza kucheza gemu hilo kupitia intaneti lakini angalau kasi yake iwe na 25Mbps.