Makampuni mengi yamekuwa yakiachana polepole kutumia vioo ya LCD na kuhamia kwenye teknolojia ya OLED lakini daima gharama za vioo hivyo imekuwa ipo juu jambo ambalo linasababisha hata bidhaa kamili kuwa ghali.
Panasonic imeliona suala hilo na kuamua kuchukua hatua ambayo itapunguza uwekezaji kwenye teknolojia hiyo; ilichokifanya kampuni hiyo ni kuunganisha nguvu (kuingia ubia) na Screen Holdings Co. Ltd.
Panasonic kazi yao itakuwa ni kuchora mchoro pamoja na kuunda kifaa ambacho kitatumika kutoa nakala mbalimbali huku upande wa pili (Screen Holdings Co. Ltd) kazi ikiwa ni kufanikisha uzalishaji wa bidhaa husika pamoja na kufanya matengenezo.
Teknolojia ya utengenezaji wa vioo ya OLED ilianzishwa na Sony pamoja na Pioneer Corp miaka ya ’90 kisha makampuni mengine yakajaribu kutumia teknolojia hiyo lakini wakaachana nayo baada ya muda kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu.