Sasa tumia moja kwa moja GIFs kwenye mtandao wa Facebook

0
Sambaza

Kwa muda mrefu wengi wameomba uwezo wa ku’post moja kwa moja video za GIFs kwenye mtandao wa Facebook lakini mtandao huo ulikuwa bado unanyima uwezo huo.

Sasa Facebook wametangaza rasmi ya kwamba uwezo huo umeanza kusambaa taratibu kwa watumiaji wake mabilioni duniani kote kwa hawamu. Kwa sasa ili mtu ku’post video/picha za mfumo wa GIF ilikuwa inambidi mtu aweke faili hilo kwenye tovuti nyingine na kisha aje Facebook na kuweka link ya GIF hiyo.

GIFs kwenye mtandao wa Facebook

Sasa tumia moja kwa moja GIFs kwenye mtandao wa Facebook

Je unafahamu GIF ni nini? Bofya kusoma makala yetu yenye historia nzima na majibu yote kuhusu video hizi.

SOMA PIA:  Facebook yawezesha kutuma picha zenye ubora wa 4K kwenye Messenger

Uwezo huo wa video za gif haujawezeshwa kwa watumiaji wa kawaida tuu bali hadi kwa wale wanaoendesha kurusa za kibiashara, yaani Pages.

Jinsi ya kupost ni kwa njia ile ile ambayo tayari inatumika kwa ajili ya kuupload picha/video katika mtandao huu maarufu wa kijamii.

Hivi karibuni tuu Facebook ilifikisha wastani wa watumiaji bilioni 2 kwa mwezi na kwa wanajitahidi zaidi kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuwafanya watumiaji hawa kuendelea kuupenda mtandao huu na hivyo kuendelea kuwavutia wengine zaidi.

SOMA PIA:  Apple yapunguza ushuru kwenye duka la apps

Vipi je wewe ni mtumiaji wa mafaili ya mfumo wa GIF? Je una mtazamo gani juu ya ujio huu?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com