Google Chrome; Sasa Unaweza Kunyamazisha Tab - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google Chrome; Sasa Unaweza Kunyamazisha Tab

1
Sambaza

Google chrome ilikuwa ndiyo kitumizi cha kwanza kuweza kumjulisha mtumiaji ni tab ipi katika kitumizi chake ambayo ina toa sauti, kumbuka kabla ya hapa ilikua tabu kujua tab ipi kati ya zile ulizozifungua ambayo inatoa sauti (hasa kama umefungua tab zaidi ya moja)

google-chrome (1)

Watengenezaji wengine wa vitumizi wameiga mtindo huo na kwa sasa karibu kila kitumizi kinao huu uwezo wa kukuonesha ni kurasa(tab) ipi ambayo inatoa sauti, shida iliyo baki kwa sasa ni kwamba hauwezi kuwa umefungua kurasa mbili au zaidi kwa wakati mmoja zenye kutoa sauti. Maana zitakuwa zinakuchanganya na utalazimika kusimamisha ukurasa mmoja.

hqdefault

Google chrome imepatiwa uwezo wa kumruhusu mtumiaji kunyamazisha baadhi ya kurasa alizozifungua na kitumizi, uwezo huu sasa utawaruhusu watumiaji kuweza kufungua kurasa zaidi ya moja zinazocheza sauti bila ya usumbufu kwa kuzinyamazisha zile ambazo haziitajiki wakati huo.

INAYOHUSIANA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Kuanza kutumia utaratibu huu mtumiaji anatakiwa kunakili amri hii  chrome://flags/#enable-tab-audio-muting katika sehemu ya anuani ya kitumizi cha google chrome na kisha kuwezesha (enable) au kukipa uwezo  huo wa kunyamazisha. Hii ni namna nyepesi zaidi ya kunyamazisha kurasa zenye sauti bila ya kuzifunga kurasa hizo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

1 Comment

  1. Pingback: Google Chrome; Sasa Unaweza Kunyamazisha Tab | Teknolojia

Leave A Reply