Google iliilipa Apple Dola bilioni 1 ili Huduma Yao ya Search kutumika katika iOS

0
Sambaza

Imegundulika kwamba mwaka 2014 kampuni ya Apple ilipokea malipo yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni moja, inaelezwa kwamba yalilipwa baada ya Apple kuiweka search bar ya Google katika iOS.

IOS

Search bar ya Google inavyoonekana katika iOS

Katika taarifa iliyochapishwa na jarida la Bloomberg jarida hilo linasema kwamba taarifa hii imepatikana katika moja ya mafaili ya kesi inayoendelea kati ya Google na Oracle Corp ambayo ni kesi ya hatimiliki. Moja ya nakala laini za mafaili ya kesi hiyo ambayo yaliwekwa kupatikana kwa umma ilikuwa na taarifa juu ya malipo hayo. Hata hivyo baada ya muda nakala ya faili hili ambalo mwanzo lilikuwa linapatikana kwa uma liliondolewa (pengine ni baada ya Google kuomba litolewe).

SOMA PIA:  Uwezekano wa kuibiwa nywila za iOS na Mac kwa kutumia 'Image file' yenye kirusi

Pengine unawaza kwanini habari hii imepata nafasi katika vyombo vya habari ulimwenguni…

  1. Kwanza ni muda mrefu kume kuwa na tetesi za kwamba Google wanawalipa Apple ili huduma yao ya utafutaji itumike katika ‘search bar’ ya kwenye iOS lakini tetesi hizi hazikuwahi kufikia level ya kuwa na ushahidi kama uliopo sasa. Hii imeifanya habari hii kuwa ndiyo ya kwanza kutoa na ushahidi wa kiasi ambacho makampuni haya hasimu yanalipana.
  2. Sababu nyingine inafanya hii habari ipate kiki kubwa ni ukweli kwamba Tim cook Mkurugenzi mtendaji wa Apple amekuwa ndiye mkosoaji juu ya jinsi Google wanavyo tumia data kutoka katika utumiaji wa huduma ya utafutaji (search) na kuzitumia hizo katika matangazo kumbe nyuma ya pazia kampuni yake imekuwa inatengeneza kiwango kikubwa cha pesa kupitia njia ambayo yeye anaipinga.
SOMA PIA:  Mkurugenzi wa Apple ameanza kutumia iPhone 8 ambayo haijazinduliwa rasmi?

Kiasi hicho cha dola za kimarekani bilioni moja ni kiasi kikubwa na kibongo bongo kingeweza kujenga barabara karibu kumi kila moja ikiwa na urefu wa kama kilomita 400.

Malipo haya ya dola za kimarekani bilioni moja ni asilimia 34 ya mapato ambayo google inayapata kwa kuweka search bar yake katika vifaa vya Apple, hii inatoa picha ni kwa kiasi gani biashara ya utafutaji (search) ilivyo na pesa nyingi.

Endelea kufuatilia mtandao wako wa TEKNOKONA kwa taarifa mbalibali za teknolojia katika lugha yetu tamu ya kiswahili, Tuandikie mawazo maswali ama maoni nasi tutajibu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com