Google Inanunua Sehemu Ya Timu Nyuma Ya Simu Za HTC! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google Inanunua Sehemu Ya Timu Nyuma Ya Simu Za HTC!

0
Sambaza

Baada ya fununu nyingi kuzagaa kuwa Google iko katika mchakato wa kununa kampuni ya HTC, mambo yamewekwa wazi na haya ndio yaliyojiri.

http://intrepidnortheast.com/tag/conway/

source Google hainunua kampuni ya HTC bali inanunua sehemu ya timu ya HTC katika upande wa simu. Hii inaonyesha dhahiri kuwa kampuni ya Google inataka kuboresha sehemu yake ya simu ( Simu za Pixel).

http://carlsonschimney.com/chimney-cleaning/

Hii sio mara ya kwanza Google kununua kampuni nyingine ya simu kumbuka mara ya kwanza ilinunua Motorola na baadae kuiuza kwa Lenovo.

Ununuzi huo wa Google kwa HTC ni wa dola bilioni 1.1 za kimarekani. Pengine labda HTC imekubali kuuza sehemu hiyo ya time yake baada ya kuona kuwa kuna ushindani mkubwa sana katika soko. Labda imeona ni vigumu kuioita Apple, Samsung na Huawei.

INAYOHUSIANA  Google Classroom yaboreshwa

Lakini mkataba huu hauwazuii HTC kwa lolote, Yaani kampuni inaweza ikaendelea kuzalisha simu, bado inaweza kuendelea kuajiri watu wengine n.k

Na kama ulikua hujui bado kampuni iko katika maandalizi ya kuachia simu yake nyingine ambayo itakua kidedea katika zile za kampuni hilo.

Kumbuka kampuni ya HTC ndiyo iliyotengeneza simu za Google Pixel na Pixel XL

Simu Za Google Pixel Na Pixel XL

Kwa haraka haraka inawezekana kuwa Google wamenunua ile timu ambayo ilitengeneza simu zao za Pixel tuu. Hili ni jambo zuri kwani kampuni inaweza ikafanya mambo makubwa zaidi katika utengenezaji wa simu zijazo.

Ningependa kusikia kutoka kwako, je kwa mtazamo wako unadhani simu mpya zitakazotoka Google zitakua ni tishio kwa Apple na Samsung? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila SIku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.