Google Inaweza Ikabadilisha Muonekano Wake Katika Simu Janja!

0
Sambaza

Google ndio mtandao unaoongoza kutembelewa duniani, Kwa miaka kadhaa umekua ukiwapa watu majibu ya vitu wanavyotafuta.

Muonekano wake umezoeleka na ua sifa kubwa ya kuwa na vitu vichache katika tovuti yake (website) huku rangi nyeupe ikitawala eneo kubwa.

Kulingana na mabadiliko ambayo yalionekana katika iOs na baadae yakaonekana katika Android inaonyesha dhahiri kuwa Google iko katika mchakato wa kubadili muonekano wake.

airtel tanzania bando

Mabadiliko haya ya muonekano yanafanyika ili kuhakikisha kuwa watu wanapata kile kizuri kabisa wakati wakiwa wanatafuta (search) vitu katika mtandao huo.

SOMA PIA:  Apple Kuongeza Dau Kwa Google Ili Kubakia Kuwa Sehemu Kuu Ya Matafuto (Default Search Engine) Katika iOS!

Kwa haraka haraka ni kwamba muonekano mpya kwa kiasi kikubwa unafanana kama ule wa Google Now. Majibu yanatokea kama kwenye kiboksi hivi.

Link ya mtandao husika kuanza kuonekana kwa juu kabisa katika kiboksi husika wakati kwa zamani zilikua zinaonekana pale chini mwishoni.

Baadhi Ya Vitu Katika Muonekano Mpya Wa Google

Pia vile vile kuna vidoti vyenye rangi tofauti tofauti ambavyo vinatokea upande wa kulia mwa link husika. Japokuwa mpaka sasa bado haijajulikana maana ya doti hizo ni nini lakini inaweza ikawa inatoa taarifa fulani kuhusiana na hiyo link kwani sio kama doti hizo zinatokea kwa kila link.

SOMA PIA:  Ndege ya huduma ya intaneti kutoka Facebook yapata ajali ktk majaribio

vile vile chanzo kinasema kuwa kutakuwa na matokeo machache ya tafiti zilizolipiwa (paid Ad search result) kwa juu. Awali tulizoea kuona tatu mpaka tano kama sijakosea hivyo namba hii inaweza ikashuka muda wowote.

Inasemekana kwa watumiaji wa Android watachelewa kupata muonekano huu mpya. Ukiachana na yote hayo hili ni jambo zuri kutoka Google kwani wanaboresha jinsi mtu anavyoweza tafuta vitu katika mtandao wao

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com