Google I/O kufanyika Mountain View California - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google I/O kufanyika Mountain View California

0
Sambaza

Mkutano mkubwa wa Google kwa watengenezaji wa apps unaoitwa Google I/O unatarajiwa kufanyika tarehe 18 hadi 20 ya mwezi Mei katika jiji la California lakini katika mji wa Mountain View ambapo ndipo ulipofanyika wa kwanza miaka 10 iliyopita.

google i

Mkurugenzi Mtendaji wa Google Sundar Pichai

Mkurugenzi mtendaji wa Google amesema kwamba mkutano wa Google I/O huu utahama mahali ulipofanyika mara ya mwisho na kusogea Silcon valley katika eneo kubwa zaidi ambalo litaleta hisia za enzi za mwanzo za kampuni hiyo miaka kumi iliyopita wakati kampuni hii inaanza.

Ukumbi ambao mkutano huu utafanyika mwaka huu unauwezo wa kuchukua watu takribani 25000, ambayo inaweza kuruhusu wageni 7000 zaidi ya wale waliohuzulia mwaka jana.

INAYOHUSIANA  Honor 9N yazinduuliwa

Mkutano huu wa Google I/O hutmiwa sana kwa ajiri ya kuonesha teknolojia zinazokuja kutoka kwa kampuni ya Google. Moja ya mambo mengi ambayo yanatarajiwa katika mkutano huu ni toleo jipya la Android ambalo halijapewa jina bado (soma hapa)

Google-I-O-2016-800x500_c

Ingawa mkutano huu wa Google I/O ni kwa ajiri ya watengenezaji wa vitumizi vya Google lakini ukweli ni kwamba kila mtu anauongelea na kuufatilia kwa sababu Google wamejenga tabia ya kutangaza na kuonesha bidhaa mpya hapa kama vile ilivyo kuwa kwa Android TV.

Teknokona itaendelea kukupatia taarifa juu ya mkutano huu kadiri zinavyotujia, hivyo endelea kuwa nasi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply