Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

0
Sambaza

Masasisho ni muhimu sana katika vifaa vya kieletroniki (simu, tabiti, kompyuta, n.k) katika kusaidia kifaa kiwe salama dhidi ya udukuzi, virusi lakini Google itafikia tamati kutoa masasisho kwa simu janja Pixel na Nexus.

Kampuni mbalimbali (ikiwemo Google) zimekuwa zikitia masasisho mbalimbali kwa simu zao ili kusaidia simu hizo kuwa na ulinzi madhubuti na hivyo kuzifanya kuzidi kuwa salama dhidi ya waalifu wa mitandaoni, virusi na wengineo.

Kuacha kutoa masasisho kutaathiri nini?

Kuacha kwa Google kutoa masasisho inamaanisha kuwa watuaji wa simu husika hawatopata msaada wa papo kwa papo kupitia tovuti husika ya kampuni iliyotengeneza simu husika, kutopata masasisho ya kiusalama kwa ajili ya kuzuia udukuzi lakini pia kukosa masasisho ya kawaida dhidi ya virusi, n.k.

SOMA PIA:  Samsung Galaxy S9 Itakuja Katika Matoleo Mawili!

Je, tamati ya simu hizo kupokea masasisho ni lini?

Kwanza, ni vyema kujua simu ambazo zitaathiriwa na kitendo cha Google kuacha kutoa masasisho. Simu janja, Pixel na Pixel XL ambazo hazina muda mrefu tangu ziingie sokoni baada ya kuingizwa sokoni mwaka 2016 zitapata masasisho ya programu endeshaji (Android) mpaka Oktoba 2018 na kupata masasisho kwa ajili ya usalama wa simu mpaka Oktoba 2019. Hii itajumusha na kuacha kutoa msaada wa papo kwa papo kupitia mtadaoni.

SOMA PIA:  Rasmi: Uzinduzi wa iPhone 8 kufanyika Septemba 12 mwaka huu

Soma pia: Fahamu kuhusu Pixel na Pixel XL; simu janja kutoka Google

simu Google pixel

Simu za Google Pixel kutoka Google

Mountain View nao wataacha kutoa msaada (masasisho) kwa simu iliyo chini ya Huawei, Nexus 6P pamoja na simu janja iliyo chini ya LG, 5X ifikapo Septemba 2018 (mwaka mmoja baada ya kuacha kupata masasisho ya kwenye programu endeshaji). Kama unamiliki Nexus 6 au  basi tambua kuwa mwezi Oktoba 2017 ndio itakuwa mwisho wa kupokea masasisho kwa ajili ya usalama wa simu yako.

SOMA PIA:  Mkutano wa pili wa Africa Open Data waanza nchini Ghana

Soma pia: Simu janja ijulikanayo kama Nexus kutoka Google 

Simu za google nexus

Nexus ni moja ya simu janja ambapo wakati zilipokuwa zinatoka mwaka 2015 bei yake ilianzia $499 (zaidi ya Tsh. 1,097,800).

Kama kawaida yetu TeknoKona tumeshakuhabarisha sasa imebaki wewe kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Usiache kuwa karibu nasi kwa kutufuatilia kupitia Facebook, Instagram halikadhalika Twitter.

Chanzo: Engadget

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com