Google Kuanza Kutengeneza “Chip” Zao Kwa Ajili ya Android

0

Sambaza

Ndio! mpaka sasa Google bado hawajaanza kutengeneza chip za kwao kwa ajiri ya mfumo endeshi wa Android ambao wao ndio wanautengeneza, badala yake Google wanatumia chip zinazotengenezwa na makampuni mengine kama Samsung na Qualcomm.

Imesemekana kwamba Google wataanza kutengeneza na kubuni chip zao wenyewe ili kuweza kupambana na mahasimu wao wakubwa Apple, ambao ndio watengenezaji wa mfumo endeshi wa iOS ambao unatumiwa na vifaa vya Apple.

Chip ya A9 ambayo hutumiwa na APPLE katika moja ya vifaa vyake

Kwa mujibu wa jarida la teknolojia la The information ni kwamba Google wanataka kufanya hivi ili waweze kuweza kubuni na kutengeneza simu janja ambazo zina uwezo zaidi ilivyo sasa, kufanya hivi basi watahitaji kuanza ubunifu kuanzia katika hatua ya utengenezaji wa chip ambazo ndio kiini hasa cha ufanyaji kazi wa simu.

INAYOHUSIANA  Muonekano wa giza unapunguza matumizi ya betri

Hii inamaanisha kuwa Google watahitaji kushirikana na watengenezaji maarufu wa chip ili waweze kushirikiana nao kutengeneza chip za Android ambazo zimebuniwa na wataalamu wa Google, pia wanaweza kuinunua kampuni ndogo ya utengenezaji wa chip na wao kuingiza wataalamu wao katika utengenezaji huo.

Hatua hii inafungua ukurasa mwingine katika mapambano ya hawa mahasimu wakubwa wawili katika utengenezaji wa simu janja, na pengine itachangia kwa kiasi kikubwa simu za Android jinsi zitakavyo kuwa zinafanya kazi siku zijazo. Hatua hii inasemekana itawasaidia Google kutengeneza mfumo endeshi ambao utakuwa na uwezo wa Virtual Reality ambayo ni moja ya vitu vinaongelewa zaidi katika teknolojia hivi sasa.

INAYOHUSIANA  WhatsApp kuja na muonekano wa giza

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Leave A Reply