Google kurudi China? Inaonekana tayari wapo ktk mkakati huo - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google kurudi China? Inaonekana tayari wapo ktk mkakati huo

0
Sambaza

Kuna uwezekano mkubwa kwamba viongozi wa Google wanampango wa kurudisha huduma katika nchi ya China baada ya kufunga huduma zake katika nchi hiyo kwa takribani miaka 6.

http://canhamfarm.com/?wpsc_action=rss

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Google mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo amesema wanajari kuwahudumia wateja wote popote walipo.

buy generic ciprofloxacin sundar-pichai-google-ceo-e1439335509776
China ni moja kati ya nchi ambazo zinasheria kali za mitandao, serikali ya nchi hiyo huyalazimisha makampuni ya mitandao kuchuja mambo yanayowafikia watumiaji wa kawaida hii ilipelekea kwa baadhi ya makampuni kama Google kuacha kutoa huduma katika nchi hiyo ya kikomunisti.

buy flagyl/generic metronidazole Google iliondoka China mwaka 2010 huku ikiacha soko ambalo lina watumiaji wengi zaidi  wa mtandao na ambao wanakua kwa kasi kushinda sehemu yeyote, kurudi kwa Google China kutaisaidia zaidi katika mapambano yake na mitandao mikubwa mingine kama vile Facebook ambao nao tayari wameanza juhudi za kutaka kurudi nchini humo. Facebook wamebaniwa huduma nchini humo tokea 2009.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Ingawa Google iliondoka Uchina mwaka 2010 lakini bado imekuwa muda wote huo Hong Kong ambako sheria zidi ya mitandao ni kwa kiasi fulani rahisis ukilinganisha na China bara.

Katika habari nyingine mkurugenzi mtendaji wa Google ametumia muda mwingi kuongelea “Artificial Intelligence” wakati akitoa maada katika mkutano ulioandaliwa na kampuni hiyo, inasemekana kwamba kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kutafuta mambo katika google kwa kutmia sauti zaidi ya nyia ya zamani ya kuandika kitu kwa kutumia keyboard.

Kwa ujumla sekta ya “artificial intelligence” inawigo mpana zaidi hasa katika nyakati hizi ambapo watumiaji wa mifumo mingi wangependa kuwa na mifumo  ambayo inafanya kiasi kikubwa cha kazi yenyewe.

INAYOHUSIANA  Miaka kumi ya App Store kwenye biashara

Kwa inavyoonekana ni kwamba Google imegundua kwamba ili ibaki kuwa mtandao unaopendwa zaidi basi hawana budi kubadilika na kuacha kufanya kazi kama ambavyo walikuwa wanafanya na kwenda na mabadiliko – ata kama ni magumu kumeza 🙂 .

Endelea kutembelea Teknokona kwa habari zaidi za teknolojia kwa katika lugha yako adhimu ya kiswahili.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.