Google kusitisha uungwaji mkono wa app za Chrome kwa linux Mac na Windows

0
Sambaza

Kampuni ya Google imeamua kusitisha uungwaji mkono wa apps za Chrome kwa OS za Linux, Mac na Windows katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Hii inamaana kwamba baada ya miaka miwili basi watumiaji wa kivinjari cha Google Chrome ambao wanatuma apps za Chrome hawataweza kuzitumia tena.

apps za chrome

Uungaji mkono unamaana gani?

Tunaposema kusitishwa uungaji mkono hii inamaanishwa kwamba Google hawatajiuhusisha tena na utengenezaji ama kusaidia kutatua matatizo ya app hizo katika OS tajwa pindi itakapofika wakati huo. Hii ina maanisha kwamba itakapofika mwaka 2018 watumiaji wa kivinjari cha Google Chrome katika OS za Linux Mac na Windows hawatakuwa wanatumia app hizi tena.

SOMA PIA:  Datally, app kutoka Google: Njia ya kuokoa utumiaji data wa apps kwenye simu yako

Kwanini Google wanafanya hivi?

Google wanasema kwamba wanaachana na apps hizi kwa OS tajwa kwasababu matumizi yake yamepungua sana kitu ambacho kimesababishwa na uboreshwaji wa web app hivyo kuzifanya app za Chrome kutokuwa na umuhimu sana.

airtel tanzania bando

Nini kitatokea kwa watumiaji wa Google Chrome?!

Kwa watumiaji wa Google Chrome hata hivyo wataendelea kuzipata na kuzitumia app hizi kwa kuwa Google wanasema kwama app za Chrome ni muhimu kwa ufanyaji kazi wa kivinjari cha Chrome. Na pia watumiaji wa kompyuta zinazotumia programu endeshaji ya Chrome OS, yaani Chromebooks, wataendelea kupata apps hizo bila tatizo lolote.

SOMA PIA:  Namna gani unaweza kupakua video/picha kwenye Instagram

Vyanzo: mtandao wa Gadgets360 pamoja na mitandao mingine ya Teknolojia

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com