Google kutambulisha simu janja mbili mwezi Oktoba - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google kutambulisha simu janja mbili mwezi Oktoba

2
Sambaza

Katika suala zima la biashara za simu janja ama kwa hakika naweza kusema ni “vita” ambayo haijulikani ni lini itafikia ukomo. Sasa Google nao wapo njiani kutambulisha Pixel 2 na Pixel 2 XL.

Baada ya Apple na Samsung kutambulisha simu zao ambazo zinasemekana kuwa gumzo kutokana na mambo kadha wa kadha yaliyomo kwenye simu janja hizo Google nao hawajataka kuwaacha wapenzi wa bidhaa za Google wakisubiri sana kitu ambacho imewaandalia wateja wake na ulimengu mzima kwa ujumla.

here Simu janja za Google Pixel ni muendelezo tu simu hizo kutoka familia moja, yaani Pixel ambapo toleo la nyuma yake lilisifika sana kwa kamera yenye ubora na hata kupata tuzo mbalimbali.

INAYOHUSIANA  Mkebe wa kuhifadhi AirPods kuwa na uwezo wa kuchaji iPhone

Je, ni nini kilichoboreshwa kwenye toleo jipya Google Pixel 2 na Pixel 2 XL?

>Prosesa/Kioo.

SImu zote mbili (Pixel 2 na Pixel 2 XL) zitakuwa na prosesa inayofahamika kama Qualcomm Snapdragon 835. Ukubwa wa kioo kwa Pixel 2 utakuwa ni inchi 5 kilichotengenezwa na HTC ( where can i buy aciclovir over the counter ambapo hivi sasa kampuni ijulikanayo kama HTC imenunuliwa na Google).

Pixel 2 (ya upande wa kushoto) na Pixel 2 XL(ya kulia). Kioo cha Pixel 2 XL kinafanana na kile kilichopo kwenye LG G6.

>RAM/Diski ujazo

Google Pixel 2 na Pixel 2 XL zote kwa pamoja zina ukubwa GB 4 za RAM huku zikitofautiana kwenye diski ujazo ambao ni kati ya GB 64 mpaka GB 128. http://girlsintanktops.com/tats-on-tats-on-tats/ Kuna uwezekano wa simu hizo kuja na toleo jipya la programu endeshi (Android 8).

INAYOHUSIANA  Xiaomi wazindua simu mpya Redmi 6 Pro yenye Snapdragon 625 kwa bei rahisi

>Sehemu ya kuchomekea “earphones”/USB Type C

Tangu Apple watambulishe teknolojia ya simu yao (iPhone 7) kutokuwa na sehemu ya kuchomekea spika za masikioni kampuni kama Google nao wameona si vibaya wakiitumia teknolojia hiyo kwenye simu janja mbili (Pixel 2 na Pixel 2 XL) lakini simu hizo pia zitakuwa zinatumia teknolojia ambayo pia ni maarufu sana katika miaka ya hivi karibuni, USB Type C. Kujua zaidi kuhusu USB Type C BOFYA HAPA!.

Uzinduzi wa simu zote mbili kutoka Goolge unatarajiwa kufanyika Oktoba 4, 2017 huko San Francisco huko Marekani.

>Bei/Usalama

Goolgle ni moja ya makampuni ambayo bidhaa zake kama simu janja kutokuwa ghali lakini simu janja Pixel 2 na Pixel 2 XL zinatarajia kuuzwa kati ya $849 ya GB 64 (Tsh. 1,910,250) na $949 ya GB 128 (Tsh. 2,135,250). Simu zote za Pixel 2 zitakuwa na ule mfumo wa sensa anbayo ukigusa tu kwa kidole chako basi simu yako inafunguka.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Google wamejipanga kuleta ushindani katika soko la simu janja ambalo mpaka hivi sasa linaonekana kutawaliwa na Samsung Galaxy Note 8 na iPhone 8/iPhone X. Wewe kama mpenzi wa simu janja unazinzunguziaje simu janja mpya kutoka Google?

Vyanzo: The Guardian, The Verge.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|