Google My Activity; Fahamu na Kufuta vyote ufanyavyo vilivyounganishwa na Google

0
Sambaza

Amini usiamini Google wanafahamu mambo mengi kuhusu wewe kuliko ata rafiki zako wa karibu au ndugu zako. Unakubaliana na hili?

My Activity

Google wanafahamu jana umefanya nini kwenye simu yako ya Android, umetumia app gani, umetembelea mtandao gani, umeenda wapi na mambo mengine mbalimbali kuhusu wewe.

Na sasa kukusaidia kwa urahisi kuweza kufahamu yote wanayojua kuhusu wewe Google wana huduma inayoitwa ‘My Activity’.

airtel tanzania bando

My Activity ni kitu gani hasa?

Ni orodha ya mambo yote ambayo mfumo wa Google unafahamu kuhusu ulichofanya au kutumia katika huduma zao zote – iwe mtandao au kitu katika programu endeshaji yao ya Android.

SOMA PIA:  Tengeneza chanzo cha umeme wa kuchaji simu kwa kutumia viwembe

Pia utaweza hadi kutafuta kitu husika katika orodha hiyo yenye data mbalimbali zilizopangwa kuanzia mpya hadi za zamani.

  • Mitandao uliyotembelea
  • Video ulizotazama katika huduma za Youtube
  • Apps na huduma ulizotumia kwenye simu yako ya Android
  • Vitu ulivyotafuta katika Google Search

Jinsi ya Kufuta data zako zote

Kama umeona kitu ambacho hukitaki kiwe kwenye data za Google basi unaweza kukifuta kwa kubofya eneo la doti tatu – hizi zipo pembeni kulia kwenye jambo unalotaka lifuta.

Google my activity

Je utaki Google kukufuatilia mtandaoni?

Google wamewezesha hili pia. Kama hautaki Google kuweka kumbukumbu (record) ya mambo yako basi unaweza weka ‘pause’ kupitia hapa -> https://myaccount.google.com/activitycontrols

SOMA PIA:  Twitter: Jinsi ya kuzuia au kuwezesha meseji binafsi (DM) kutoka kwa watu wote

Ukiingia kwenye linki hiyo basi utaweza chuja vitu ambavyo unataka kuwa na kumbukumbu navyo na vile ambavyo hautaki kuweka kumbukumbu katika akaunti yako ya Google. -Search, Location, video za Youtube n.k.

Je kuna faida yeyote ya Google kuwa na data hizi kuhusu wewe?

Wenyewe Google wamewahikikishia watumiaji wake ya kwamba data hizo haziuzwi moja kwa moja kwa mtu mwingine yeyote. Bali data hizo hutumika na kompyuta zao katika kuhakikisha wanakuletea matangazo ya maana kwako kutokana na tabia zako za mtandaoni (unafanya nini, unatembelea mitandao gani).

SOMA PIA:  Simu janja 7 kutoka China ambazo hazijulikani na wengi! (2017) #Uchambuzi

Pia kompyuta zao kuwa na data za kama vile sehemu unazoenda (location) zinaweza kusaidia katika kuhakikisha huduma zingine kama vile za ramani (Google Maps) na ata za utafutaji (Search) zinakuletea matoleo yaliyo na maana zaidi kwako…kulingana na sehemu/eneo/nchi uliyopo.

Vipi wewe unalionaje hili? Je ni bora kompyuta zao zitumie data zako katika kuboresha huduma inayokufikia au wewe unaona suala la usiri (privacy) ni muhimu sana?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com