Google na Facebook waibiwa mabilioni kupitia wizi wa mtandao - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google na Facebook waibiwa mabilioni kupitia wizi wa mtandao

0
Sambaza

Hata wajanja wanaweza danganyika. Imefahamika rasmi ya kwamba makampuni nguli ya mtandao, Google na Facebook waibiwa mabilioni kupitia wizi wa mtandao.

enter Katika kipindi cha miaka miwili Google na Facebook walijikuta wakilipa kiasi cha takribani dola milioni 100 za kimarekani kwa mwizi mmoja baada ya kufanikiwa kudanganya vitengo vya malipo mara kadhaa.

Ilitokeaje?

buy Mysoline online pharmacy google na facebook waibiwa mabilioni

http://macromicro.com/macromicro-sap-sapphire/_dsc6542/?share=twitter Kijana mmoja wa nchini Lithuania ambaye ameshakamatwa alifanikiwa kutuma barua pepe zikiwa zimeambatanishwa na madai ya malipo (invoice) na sahihi za mfumo wa ‘stamp’ ili kuwahadaa wafanyaji malipo ya huduma mbalimbali ambazo makampuni hayo huwa yanazipata kutoka makampuni mengine.

Na kikubwa zaidi ni kwamba alitumia taarifa zinaoonesha ni madai kutoka moja ya kampuni kubwa ya nchini Taiwani, Quarta Computer, ambayo tayari ni mtoaji huduma za aina mbalimbali kwa makampuni hayo.

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

Unaweza shangaa kama makampuni makubwa kwenye masuala ya intaneti kama Google na Facebook wanaweza ibiwa kwa njia za mtandao je wewe upo salama?

Wizi wa kimtandao unaohusisha utumiaji wa barua pepe unaweza kumkuta yeyote.ila kuna machache yanaweza kukusaidia kuwa salama;

  • Ukipokea barua pepe ambayo huielewi elewi ilipotoka basi epuka kabisa kubofya linki/url zilizondani yake
  • Kingine ni kwamba hakikisha kama umepokea barua pepe inayoonesha ombi flani na ulielewi elewi jaribu kufanya utafutaji (search) kwenye mtandao wa Google kuona kama hakuna ambao washalalamika kuhusu suala hilo hilo
  • Kama ni barua pepe kutpka mtu au kampuni unayofanya nayo kazi na inaitaji maipo flani basi hakikisha una fanya mawasiliano ya simu pia kuhakikisha hasa pale ambapo kuna mabadiliko ya akaunti ya malipo n.k
INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Zamani kabisa moja ya barua pepe za wizi maarufu zaidi zilihusisha wanaijeria wanaosema wanaitaji msaada wa kutuma pesa cha kiasi kingi ila wamekwamba sehemu ndogo na hivyo kuitaji msaada wako wa fedha ndogo kuhakikisha ilo na baadae watagawana na wewe baadhi ya pesa zao. Siku hizi wizi umekuwa wa kitofauti zaidi, watu wanadukua barua pepe za watu unaowaamini zaidi na kujaribu kufanikisha kukudanganya wewe au kampuni flani katika malipo ya namna flani.

Ni muhimu uwe makini katika utumiaji wako wa mtandao na hasa hasa kwenye barua pepe au jambo jingine lolote linalohusisha mapene yaani pesa mtandaoni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.