Google na Microsoft wakubaliana kuacha Kushtakiana

0
Sambaza

Kampuni mbili mashuhuri na zenye ushindi mkubwa, Google na Microsoft, zafanya makubaliano ya kuacha kushtakiani kwenye vyombo mbalimbali vya kisheria na kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo baina yao wenyewe.

google na microsoft

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kesi nyingi za kibiashara na kiteknolojia dhidi ya makampuni hayo makubwa huku kila mmoja, mara nyingi Microsoft, akidai kuibiwa teknolojia flani flani.

 Kesi hizi uchukua muda mrefu na pesa nyingi

Kupitia makubaliano yao mapya wote wataondoa kesi zao zote zilizopo katika vyombo vya kisheria. Microsoft wamesema wanajitoa katika kundi la umoja unaopigania usawa dhidi ya Google katika eneo la utafutaji (Search), kundi hilo linalojiita FairSearch limekuwa likiishtaki Google katika vyombo mbalimbali dhidi ya biashara yake ya Google Search.

Pia Microsoft wamesema hawajihusisha kabisa na uchunguzi na kesi inayofanyiwa kazi na chombo cha ushindani cha bara la Ulaya.

Uamuzi huu umepongezwa na wengi kwani badala ya makampuni haya kupoteza pesa nyingi katika kesi za miaka mingi dhidi ya mwingine kwa sasa wataweza kutumia muda mwingi katika mazungumzo na maelewano huku wakiendelea kukuza ushindani wa kibiashara kati yao.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Simu ndogo unayoweza 'Kuizungushazungusha'
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com