Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

0
Sambaza

Google na Microsoft wakubaliana kushirikiana na makampuni makubwa ya umiliki wa hakimiliki za muziki na filamu katika vita dhidi ya mitandao inayohifadhi mafaili mbalimbali na kuyatoa bila malipo yoyote kwa wenye haki miliki.

Mitandao hii ni pamoja na mitandao ya mfumo wa torrents, streaming na mingine mingi inayotoa huduma za kudownload bure vita kama vile miziki, muvi, magemu na programu/apps kwa ajili ya simu na kompyuta.

Je watafanya nini hasa?

Microsoft na Google wamekubali kufanya mabadiliko flani katika matokeo ya kurasa za kwanza katika huduma zao za utafutaji (yaani search) yatakayohakikisha mafaili mbalimbali ya wizi kutotokea katika kurasa za kwanza za matokeo ya search.

“Katika watumiaji sita wa intaneti duniani, mmoja huitumia kwa ajili ya kupakua vitu kwa njia zisizo rasmi.”

Ila ili tovuti iwekwe katika zuio hilo la kutotokea kwenye ukurasa wa kwanza wa matokeo ya search ni lazima iwe imeshapewa taarifa mbalimbali za kuondoa mafaili ya wizi kwenye tovuti husika, na kama haitochukua hatua basi Google na Microsoft watapewa taarifa hiyo na hivyo wao kuweka zuio kwa tovuti husika kutokea katika ukurasa wa kwanza wa huduma zao za Search.

SOMA PIA:  Ujenzi wa Darubini kubwa zaidi duniani waanza.

Tafiti mbalimbali zinaonesha ukuaji wa utumiaji wa mitandao katika kudownload vitu mbalimbali kwa njia za wizi/yaani bila malipo yeyote. Kwa mfano nchini Uingereza tuu takribani asilimia 15 ya watumiaji wote wa huduma ya intaneti huitumia kwa ajili ya kupakua filamu, miziki, vitabu na vingine mbalimbali kwa njia za wizi. Pia katika watumiaji sita wa intaneti duniani, mmoja huitumia kwa ajili ya kupakua vitu kwa njia zisizo rasmi.

Ingawa Google imetoa ushirikiano bado inasisitiza ya kwamba wao sio chanzo kikubwa cha watu kutembelea mitandao ya mafaili ya wizi.

SOMA PIA:  BarraCuda Pro: Diski uhifadhi ya ukubwa wa TB 12 kwa ajili ya kompyuta za mezani

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com