Google imeendelea kujaribu kuwateka watumiaji wa mtandao baada ya safari hii kuongeza michezo pendwa katika ukurasa wake, sasa watumiaji wa ukurasa wa Google wanaweza kucheza mchezo wa karata na mchezo wa Tic Tac Toe katika ukurasa huu.
Hii sio mara ya kwanza kwa Google kufanya kitu kama hiki, wakati ya mashindano ya Olimpiki Google walileta kitu kama hiki baada ya kuleta magemu ya michezo mbalimbali ambayo ilikuwa inafanyika huko Rio Brazil.
Soma zaidi: Shiriki Olimpiki ndogo iliyoanzishwa na Google
Google wameleta magemu mawili ambayo watu wanaweza kuyacheza katika ukurasa wao moja ni la karata ambalo limekuwa likipatikana katika OS ya Windows kwa muda mrefu, gemu jingine linaitwa Tic Tac Toe ambalo pia ni rahisi kucheza na linafurahisha.
Ili kuipata michezo hiyo basi mtumiaji anatakiwa kutafuta Solitaire ama Tic Tac Toe katika Google na gemu la mchezo husika litakuja la katika matokeo ya ulichotafuta, unaweza kubadili kiwango cha ugumu wa mchezo ama kwa mchezo wa Tic Tac Toe pamoja na yote unawezapia kucheza na rafiki yako na kufanya hivyo unabilisha katika orodha ya mpangilio.
Google wanfanya jitihada ili kuweza kupata watumiaji wa mtandao wengi zaidi kutembelea ukurasa wao, kwa kuwa na michezo inayowavutia watumiaji kutaongeza watumiaji wanaotembelea mtandao huu kila siku.