Google Street View yapata pingamizi nchini India

0
Sambaza

Serikali ya India imekataa mipango ya Google kukusanya picha za miji mbalimbali nchini humo baada ya kuona upigaji picha wa nyuzi 360 katika huduma ya Google ya Google Street View utahatarisha usalama wa maeneo nyeti.

google street view india

Gari la Google Streetview katika moja ya maeneo nchini India

Gari la Google Streetview katika moja ya maeneo nchini India

Waliongeza kuwa iwapo wangewakubalia ombi hilo ingeweza kuhatarisha usalama wa nchi kwa ujumla. Project hiyo “Google street view” inakusanya picha za muonekano wa hali ya juu ambapo itawawezesha wateja wake kuona picha hizo kwa namna ya “360 degrees view” kwa miji mbalimbali nchini India, maeneo ya watalii wanapotembelea, mito na mabonde n.k.

SOMA PIA:  Matumizi ya simu janja pamoja na 'Drones' katika kupambana na Malaria

Vitendo hivyo vya Google kukusanya taarifa mbalimbali imefanya nchi mbalimbali kuweza kuwaangalia kwa jicho la karibu.

google street view india

Mysore Palace – Muonekano wa moja la eneo la kitalii kupitia huduma ya Google Street View

Wizara ya Mambo ya Ndani ndiyo iliyokuwa na wasiwasi zaidi juu ya mpango huo wa Google kupiga picha maeneo mbalimbali India – wakisema itawarahisishia watu kama magaidi kupanga mashambulizi kwa sehemu bila ya ata wao kufika kabisa eneo husika. Shambulio la kigaidi a Mumbai la mwaka 2008 lilihusisha magaidi kufanya maandalizi yao yote kwa njia za mtandao.

SOMA PIA:  Google na Facebook waibiwa mabilioni kupitia wizi wa mtandao

Wizara hiyo imeona kuna umuhimu wa kuweka katatizo la kupiga picha maeneo mbalimbali nchini India kwa sababu ya shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2008 na kuamini kuwa magaidi hao walitumia picha mbalimbali kuweza kujua maeneo mbalimbali ya India.

Walisema kuwa iwapo ingeruhusu mpango wa Google wao kama mamlaka hawakuwa na uwezo wa kuwasimamia na hivyo ingeweza kuhatarisha usalama wa eneo husika na watu wake ndio maana wakaamua kuukataa mpango huo. Ila tayari wameruhusiwa kufanya hivyo kwenye maeneo ya kumbukumbu ya kitalii tuu.

SOMA PIA:  SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400

Kutumia huduma ya Google Street view kuona mazingira ya miji mbalimbali tembelea -> https://www.google.com/maps/streetview/

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com