Google Waanzisha Mkonge Mkubwa Wa Intaneti Chini Ya Bahari!

0
Sambaza

Google licha ya kushangaza watu wengi na teknolojia zao zilizojaa ubunifu wa kutosha bado kampuni inazidi kuhakikisha kuwa inazidi kujiboresha

Sasa wameamua kuja na teknolojia nyingine, Wameweza kuweka mkonge wa intaneti chini ya bahari. Mkonge huu una urefu wa maili 5600 na unaunganisha marekani na japan kupitia maji

shutterstock_227976844-900x506
Kebo hiyo ya faiba inaweza ikasambaza data za terabaiti (terabits) 60 kwa sekunde ambayo ni sawa sawa na Megabaiti Milioni 60 kwa sekunde (60M Mbps)

Kwa sasa uhitaji wa Wavuti (internet) umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana na hii ni kwa sababu siku hizi vifaa vingi vinakuwa vinatumia wavuti ili kuhakikisha vinapata vitu mbalimbali kupitia mtandao.
Karibia wavuti zote za nchi zilizoendelea zinapatikana kwa kupitia kebo (mikonge) ambayo ipo chini ya bahari. Inavyosemekana mikonge ile ambayo ina teknolojia ya kuwezesha kupita katika bahari ndio inakuwa ina uwezo mkubwa katika kuwasilisha huduma yake ya intaneti

SOMA PIA:  Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

Kipindi cha nyuma huduma nyingi za wavuti zilikuwa zinapatikana kwa kutumia msaada wa Satellite

Bahari Ambayo Inatumia Mkonge Huo

Bahari Ambayo Mkonge Huo Unapita

Mkonge huo utaunganisha maeneo ya Los Angeles, San Francisco, Potland na Seattle na ukijumuisha maeneo mawili huko Japan

Google hawapumziki hapo tuu bado wapo katika mchakato wa kutengeneza mkonge ambao utaunganisha Florida na Brazil ambao unategemewa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Mikonge kama hii ili kukamilika inahitaji mamilioni ya pesa, hapo Google itakuwa imetoa mamilioni ya pesa. Japokuwa vyanzo vinasema kuwa Google hawakuwa wenyewe katika kuhakikisha jambo hili lainafanikiwa. Inasemekana walipata baadhi ya misaada kutoka katika makampuni mengine ya Asia

SOMA PIA:  Ifahamu Program Endeshaji Mpya Ya Android Baada Ya 'Android Nougat!

Niandikie sehemu ya comment hapo chini je wewe hii umeipokeaje? Na unaonaje kama Tanzania ingepata inteneti ya kasi zaidi ingekuaje? Maana kwa nchi yetu tunaweza tukashangaa mitandao yote inaweza ikawa inatumia 3G lakini ukashangaa bado uwezo wa kufungua kurasa unatofautiana

Ningependa kusikia kutoka kwako. Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kwa habari na maujanja mbalimbali yanayohusu Teknolojia kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com