Google waleta App spesheli kwa Music: YouTube Music

0
Sambaza

Alphabet Inc, wamiliki wa kampuni ya Google wametambulisha App mpya maalum kwa miziki inayojulikana kama YouTube Music, siku chache baada ya kuja na Youtube Red, huduma ya Youtube ya kulipia isiyohusisha matangazo.

YouTube wametambulisha huduma yao mpya ya kulipia katikan makao makuu ya YouTube, Los Angeles, Califonia Marekani Rey,  REUTERS/Lucy Nicholson

YouTube wametambulisha huduma yao mpya ya kulipia katikan makao makuu ya YouTube, Los Angeles, Califonia Marekani Rey, REUTERS/Lucy Nicholson

App hii mpya ya kucheza miziki mtandaoni, inalenga kutumia mamilioni ya video za muziki zinazopatikana YouTube ili kuwafikia wapenzi wa huduma za sauti bila picha ili kuongeza ushindani katika soko.

SOMA PIA:  Mambo ya Kufanya Kabla ya Kuuza au Kubadilisha Simu Yako! #Maujanja

Kampuni hiyo imeelezwa kuwa, kwa kutumia App hiyo, inayopatikana kwa simu za Android na IOS, kugundua miziki mipya itakua rahisi kuliko awali, kwa mtumiaji kuweza kupata ladha tofauti za mziki anazopenda kwa mkupuo.

Kuna kitufe cha ‘Home’ pia, ambacho kitakuwa kinatumika kukuchagulia miziki utakayoweza kuipenda, kulingana na aina ya miziki utakayokuwa unaicheza kwenye App hiyo.

youtube-music

Hii ni ya kuwafikia wapenzi wa huduma za Music, hasa wakati mtu unasafiri unapohitaji sauti bila video. Ni bomba!

Zaidi ya hayo, Youtube Music pia watawawezesha watumiaji kuweza kupata mamilioni ya nyimbo na video kutoka kwa wasanii mbalimbali duniani huku vikiambatana na picha za makasha yya Albamu, video fupi za matamasha ya mziki huo na video za ‘lyrics’ pia.

SOMA PIA:  Matangazo kwenye simu: Jinsi ya kuzuia matangazo kwenye simu za Android

Google wameeleza kuwa, utaweza kutumia YouTube Music bila matangazo yeyote, au kudownload miziki na kuisikiliza baadae hata kama kifaa hakitakuwa hewani, lakini kwa masharti ya kuboresha kwenda huduma ya YouTube Red inayolipiwa takribani Dola 9.99 za kimarekani kwa mwezi.

Youtube Music IOS

Kurasa za mbele za Youtube Music zinaonekana kama za Youtube ya kawaida, japo midunndo ni tofauti!

Youtube Music ni ya bure, na unaweza kuishusha kwa kubonyeza hapa kwa watumiaji wa IOS na watumiaji wa Android wanaweza kuipata kwenye Playstore. Utapewa siku 14 za majaribio, kama ukishindwa kulipia, basi utatumia bure kwa masharti ya kupata matangazo kwanza kabla ya kucheza nyimbo.

SOMA PIA:  Mwanamuziki 50 Cent atengeneza mabilioni kupitia fedha za kidigitali! #BitCoin

Chanzo: Google

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com