Michepuko basi! Google waleta Trusted Contacts app itakayoonesha ulipo! πŸ˜‚

0
Sambaza

Je unahisi mpenzi wako ama mtu wa karibu sio mkweli hasa juu ya mahali alipo? Unadhani anakudanganya yupo kazini ama darasani lakini kumbe yupo kiwanja na washkaji ama yupo na mchepuko? Usijali umepata dawa na dawa hiyo ni app ya Trusted Contacts.

Trusted Contacts

Muonekano wa app hiyo wakati mtu anataka kujua ulipo.

App hii itafanyaje kazi!?

App hii amabayo kimsingi itakuruhusu kuchagua namba kadhaa za simu ambazo zitapewa uwezo wa kupata location yako katika simu, unaweza kuamua kusambaza location yako ama moja kati ya namba ulizoweka kama trusted contact inaweza kuomba taarifa za mahali ulipo na kupewa (iwapo hautazuia ombi hilo).

SOMA PIA:  Simu za Samsung Galaxy kuanza kupata toleo la Android Oreo 2018

App hii inaweza kutumika katika nyakati mbili kama ifuatavyo

  • Ukiwa katika matatizo

Kwa mfano upo katika jengo la ofisi yenu na kuna moto umeshindwa kutoka unaweza kusambaza location yako hii itawasaidia ndugu zako kuweza kusaidia ukaokolewa kwa haraka zaidi.

airtel tanzania bando

  • Ukipotea mitaa

Mara nyingi tunaenda mitaa ambayo hatuifahamu vizuri na kupotea sio jambo geni ( labda kama unapotea mtaa huo huo kila sikuΒ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚) ukijikuta katika mtaa umepotea na unaona noma kuonekana mshamba kwa kuuliza basi unaweza kumtumia ramani ya ulipo mtu anayeifahamu mitaa vizuri kisha yeye atakuelekeza.

SOMA PIA:  Alphabet yapeleka WiFi Puerto Rico kwa mfumo wa maputo yanayopaa

trustedcontacts2

Je ni kweli kwamba Google wameleta hii App ili kutokomeza michepuko!?

Ni dhahiri kwamba Google wamehamasishwa na juhudi za Facebook ambao walileta huduma ya Safety checkΒ ambayo kimsingi ni huduma kwaajili ya watumiaji walio katika maeneo yaliyokumbwa na majanga kama tetemeko ambapo huweza kuwajulisha marafiki kwamba wapo salama.

Hii ni app kwaajili ya kina nani hasa?

Hii app inatabiriwa kuwa itapendwa na wazazi ambao wangependa kufuatilia nyendo za watoto wao, pia kwa wapenzi ambao kidogo wana wivu na wenza wao ama ambao wanahisi wapenzi wao sio waaminifu ( kaeni tayari wenyemichepuko wake kwa waumeΒ πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚)

SOMA PIA:  Hatimaye mwanzilishi wa Android azindua simu yake ya Essential

Ili kufanya kazi vizuri app hii basi inahitaji wewe na hao watu unataka uweunapata taarifa zao muwe mmeipakua na kuiweka app hii katika simu zenu. Iwapo simu itazima kwa kuishiwa betri ama kukosekana mtandao ulipo basi app hii itatuma taarifa za mahali ulipokuwepo mwisho kabla simu haijazima.

Vipi utapakua hii app? Na je, unaona hii app itapunguza watu kuchepuka? ama ndio itasababisha ugomvi katika mahusiano? tuambie katika maoni!?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube,Β Telegram naΒ Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com