Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

0
Sambaza

Simu ya kwanza ya Pixel ililetwa Oktoba mwaka 2016, na kwa kiasi flani ni simu zilizopata mafanikio flani. Inasemakana Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017.

Data za mauzo zilizotolewa na shirika linaloheshimika kwa data, IDC, zinaonesha Google waliuza simu za Pixel milioni 3.9 kwa mwaka jana. Ukilinganisha Apple wanauza zaidi ya iPhone milioni 4 kila wiki – kwa mwaka 2017. Soko zima la simu liliuza takribani simu bilioni 1.5 kwa mwaka 2017.

SOMA PIA:  Samsung yazinduliwa rasmi kwa nchi za Afrika nchini Kenya

Simu za Pixels zimesifika sana katika eneo la kamera na ubora wa picha. Google wanahakikisha simu hizo zinapata masasisho mbalimbali kwa wakati.

Ila mauzo hayo ya simu za Pixels ni mazuri kwani kwa mlinganisho ni ukuaji wa mara mbili ukilinganisha na mauzo ya mwaka 2016. Pia simu za Pixels zinashikilia asilimia 2.8 ya soko la simu nchini Marekani, hii ni ukuaji kutoka asilimia 1.8 ya mwaka mmoja nyuma.

Google kwa sasa ndio wamewekeza zaidi katika utengenezaji simu na hii ni baada ya kutumia zaidi ya bilioni 1 za kimarekani kununua timu kubwa ya wabunifu na waandisi wa mambo ya simu kutoka kampuni ya HTC.

Muonekano wa simu za Google Pixels. Timu hii iliyonunuliwa ndio ilikuwa imehusika zaidi katika ubunifu wa simu hizi kwa ushirikiano na Google.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com