Google Waondoa Uwezo wa Watu Kufanya Mabadiliko Ktk Google Maps

0
Sambaza

Hivi karibuni kuna mtumiaji mmoja wa Google Maps alifanikiwa kuchora mdoli rasmi anayewakilisha Android anayefahamika kwa jina la Droid akikojolea alama rasmi inayowakilisha kampuni ya Apple. Aliweza kuchora mchoro huo kwenye programu rasmi ya mtandaoni ya ramani inayomilikiwa na kampuni ya Google ifahamikayo kwa jina la Google Maps.

Picha @TNW

Picha @TNW

Baada ya tukio hilo inaonekana kampuni ya Google ikaamua kukaa chini na kutafakari ni jinsi gani uwezo wa mtu yeyote kuweza kufanya mabadiliko makubwa katika mtandao huo unaweza kuleta madhara ya kimahusiano dhidi ya makampuni, watu au mashirika mengine. Baada ya kuliangalia hilo wameamua kuondoa uwezo huo, kuanzia sasa si kila mtu anaweza kwenda na kufanya mabadiliko makubwa katika huduma hiyo ya Google Maps.

SOMA PIA:  AppStore: Apple yaondoa VPN kwa simu za iPhone nchini China

Google ilikuwa inaruhusu watu mbalimbali kuweza kufanya mabadiliko kama vile kuweka barabara, madaraja na vitu vingine kupitia huduma yao ya Map Maker (yaani kitengeneza ramani). Utengenezaji huu ni sawa na jinsi mfumo wa mtandao wa Wikipedia unavyofanya kazi, yaani mtu yeyote anaweza kufanya mabadiliko na kuongeza habari mbalimbali.

Ukitoa suala la mtu aliyechora katuuni ya Android ikikojolea Apple kuna mwingine ambaye ashawahi kuandika jina la Edward Snowden kama sehemu ya ikulu ya Marekani maarufu kwa jina la White House (Bwana Snowden ni mtu aliyevujisha siri kubwa na nyingi za shirika la kijasusi la nchini Marekani, CIA, aishiye Urusi kwa sasa).snowden-whitehouse-2

SOMA PIA:  WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

Kuanzia sasa Google wamesema watakuwa wanapitia kila marekebisho yakiandikwa na watu kabla ya kuruhusu yaonekane, wamedai uhamuzi umefanya mabadiliko kuchelewa kutokea kutokana na maombi kuwa mengi na hivyo tayari wameanza kufanya kazi ya kutengeneza programu ya kikompyuta ya kuweza kupitia vitu na maneno yanayowekwa na watu kabla ya kuruhusu vitu hivyo kwenye huduma hiyo ya Google Maps.

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com