Google yafanya mabadiliko muonekano wa tovuti yake katika simu janja

0
Sambaza

Kama utaamua kutafuta kitu kupitia tovuti maarufu ya Google bila shaka utaona kuna tofauti wa muonekano wa ukurasa wake katika siku chache zilizopita.

Tofauti hiyo utakayoiona ni mabadiliko yaliyofanywa na wenyewe Google katika kuboresha ukurasa wake. Mabadiliko hayo yanapatikana kwa watumiaji wa simu janja wa mifumo endeshi ya Android na iOS. Kwa watumiaji wa kompyuta hakuna mabadiliko hayo.

Muonekano mpya katika sehemu kutafuta kitu kwenye Google.

Mabadiliko hayo utayaona katika boksi lake la msingi la utafutaji wa vitu mbalimbali ambapo sasa pembeni kumekuwa na mkunjo wa mviringo badala ya muonekano wa awali ambapo kulikuwa na ncha kali bila ya mviringo. Na kisha utaona mabadiliko mengine pale utakapo tafuta kitu na yatakapokuja majibu ya kile ulichotafuta utaona matokeo yote ya utafutaji yapo ndani ya mzunguko wa boksi maalum.

Muonekano wa tovuti ya Google ukitafuta simu kupitia simu janja.

Jaribu kuingia Google kupitia Simu Janja yako ushuhudie maboresho hayo kutoka ukurasa maarufu zaidi duniani wa kutafutia vitu mbalimbali. Endelea kufatilia TeknoKona kwa kupata kila taarifa inayohusiana na mambo ya teknolojia popote duniani.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Milioni 7 wakosa huduma za simu baada ya shambulizi la kimtandao Venezuela
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com