Google kuleta mabadiliko kwa watumiaji wa simu.

0
Sambaza

Kampuni ya Google imefanyia mabadiliko mtandao wake pamoja na app ya Google, mabadiliko haya pamoja na yote yataruhusu sasa watu kutafuta vitu kwa kutumia stika na pia muundo wa app na mtandao huu vimeboreshwa.

mabadiliko

Muonekano mpya wa app hiyo ya Google

Muundo wa app na mtandao huu kabla ya maboresho haya ulikuwa rafiki zaidi kama unatafuta kitu fulani maalumu lakini changamoto ilikua inakuja pale ambapo mtumiaji wa mtandao anataka kutafuta juu ya maada fulani kwa ujumla. Mfano pale unapotafuta katika mtandao juu ya Siagi badala ya kuandika neno zima Siagi sasa mtumiaji ataweza kubonyeza stika ya siagi na mtandao kuleta taarifa husika.

mabadiliko

Mfano wa stika hizo

Mabadiliko haya yatawafanya watumiaji kutumia stika badala ya kuandika maneno pindi wanapotafuta juu ya vitu mbalimbali katika mtandao, hata hivyo sio kila neno litakuwa na stika ila ni kwa baadhi ya maneno kama vile migahawa mahoteli viwanja michezo ama hali ya hewa.

SOMA PIA:  Ifanye akaunti yako ya Facebook kuwa salama kwa kuondoa programu usizozihitaji

Mabadiliko haya ni kwa mtandao wa Google kwa watumiaji wa simu na tableti pia kwa watumiaji wa app za google kwa mfumo wa Android na iOS. Toleo hili jipya limeanza kuonekana kwa baadhi ya watumiaji walio katika nchi za ulaya na Marekani, pengine itachukua muda kidogo kufikia katika nchi zetu.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com