Google yaongeza lugha ya kiswahili katika voice search - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Google yaongeza lugha ya kiswahili katika voice search

0
Sambaza

Kampuni ya Google imetangaza uzinduzi wa lugha 30 za sehemu mbalimbali duniani zitakazoweza kutumika katika kipengele chake cha Voice search na lugha ya kiswahili ikiwemo.

http://vivianreed.com/events/list/?tribe_event_display=past Voice search hutumika katika Android na iOS kumsaidia mtu kuweza kutafuta kitu bila ya kubonyeza au kuandika na badala yake anazungumza kwa lugha ambayo imeorodheshwa na Google.

Lugha zilizoongezwa ni;

 • Amharic (Ethiopia)
 • Armenian (Armenia)
 • Azerbaijani (Azerbaijani)
 • Bengali (Bangladesh, India)
 • English (Ghana, Kenya, Nigeria, Tanzania)
 • Georgian (Georgia)
 • Gujarati (India)
 • Javanese (Indonesia)
 • Kannada (India)
 • Khmer (Cambodian)
 • Lao (Laos)
 • Latvian (Latvia)
 • Malayalam (India)
 • Marathi (India)
 • Nepali (Nepal)
 • Sinhala (Sri Lanka)
 • Sundanese (Indonesia)
 • enter site Swahili see (Tanzania, Kenya)
 • Tamil (India, Singapore, Sri Lanka, Malaysia)
 • Telugu (India)
 • Urdu (Pakistan, India)
INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa

Kuanzia sasa watumiaji wataweza kutafuta vitu kwa lugha hizo.

voice search googe

Kupitia Google Voice Search inakuwa si lazima mtumiaji wa huduma ya Google kuandika, anaweza kuongea na Google ikamuelewa anataka kutafuta nini

Lugha hizo pia zitapatikana katika Google search katika mfumo wa iOS. Kwa mujibu wa Google kutumia sauti kutafuta kitu ni njia ya kasi zaidi ya mara tatu kuliko ile ya kuandika.

Kuongezwa kwa lugha ya kiswahili na Amharic (Ethiopia) ambazo ni lugha maarufu Afrika kumeelezwa kutaongeza watumiaji wa Voice search.

Kwa miaka ya karibuni lugha ya kiswahili imeendelea kupata waongeaji wengi duniani na kuanza kufundishwa katika vyuo vikuu mbalimbali katika nchi kadhaa barani Afrika, Ulaya na Asia.

INAYOHUSIANA  Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

Unaonaje lugha ya kiswahili kuwa miongoni mwa lugha zinazopatikana katika Voice Search ya google? Tuandikie maoni yako hapo chini.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.