Google yaruhusu mtu kuweza kutengeneza “Google Maps” zake na kuzisambaza

0
Sambaza

Google Maps imekuwa msaada mkubwa sana kwa wale wote ambao wanakwenda au wanataka kwenda sehemu ambayo hajawahi kuifika/kutoifahamu kabisa. Sasa Google imeamua kurahisisha mambo kwenye Google Map.

Katika masasisho ambayo yalianza kupatikana mapema mwaka huu huu ila si wengi wanaojua hasa kwa nchi za Afrika ni kwamba sasa hivi Google inaruhusu kutengeneza orodha (kwenye Google Map) ya sehemu ambazo unapenda kuzitembelea/umeshawahi kuzitembelea na kisha kuweza kusambaza kwa wengine (ndugu, jamaa, marafiki).

Maana yake ni kwamba utaweza kukusanya sehemu moja maeneo mbalimbali ambazo umeshawahi kufika au una mpango wa kufika hapo na kisha kuweza kuwashirikisha na wengine jambo linaloweza kupelekea na wao wakafikiria kutembelea maeneo hayo.

Namna ya kutengeneza orodha ya sehemu ulizowahi kuzitembelea/una mpango wa kuzitembelea.

Hatua ni chache na rahisi kueleweka ila usipokuwa makini kwenda hatua baada ya hatua unaweza ukaona ni kitu kigumu sana kukifanikisha. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

  • Fungua Google Map
  • Bofya menyu kuweza kutafuta sehemu ambazo umezitembelea au una mpango wa kuzotembelea
  • Bofya “Save” kuweza kuhifadhi sehemu ambazo umezichagua.
SOMA PIA:  Balaa la udukuzi wa Mitandao waikumba Dunia! #WannaCry

Kama unataka kutengeneza orodha mpya, fungua kwenye orodha ya sasa na kisha bofya ‘New list’ kuweza kutengeneza orodha mpya kisha unaandika jina ambalo unataka kuiita orodha hiyo mpya unayoitenengeneza halafu unabonyeza ‘Create’.

Hatua kwa hatua namna gani unavyoweza ukatengeneza orodha ya sehemu ambazo unataka kuzitembelea uzione dhahiri zilivyo au umeshawahi kuzitembelea. Oia unaweza ukatengeneza orodha mpya kutokana na orodha ilyopo.

Jinsi ya kusambaza orodha ya mahali uliyokwishaitengeneza.

Baada ya sasa umesharidhika na orodha ambayo umeitengeneza kwenye hatua iliyopita na una dhumuni la kuwashirikisha na wengine wajue ni wapi umeshawahi kutembelea au ambapo una mpango wa kupatembelea itakubidi ufuate hatua zifuatazo uweze kufanikisha:-

  • Fungua Google Map
  • Bofya menyu kisha chagua Your placeskutoka kwenye menyu ndogo itakayojitokeza, utaenda kwenye kipengele cha Savedkuweza kuona orodha zotte ambazo ulizitengeneza,
  • Utabofya Share listna kisha bofya Continue‘. Hapo utakuwa umetengeneza link kwa yeyote ambaye utaisambaza na akaifungua link husika basi ataweza kuona orodha yako ya sehemu ambazo umeshawahi kuzitembelea au utazitembelea katika siku zijazo.

    Unaweza pia ukahariri orodha uliyoitengeneza kwa kuchagua Edit listkutoka kwenye orodha ndogo au hata ukaamua kuificha orodha yenyewe (hide on your map) kitu ambacho kitawezesha kutengeneza orodha ya watu wa kuwasambazia bila kitu husika kutokea.

    Unaweza kuamua kuifanya orodha yako iwe wazi (mtu akiitafuta kwenye Google aweze kuipata); unaingia kwenye “Sharing options” halafu unachagua “Public”.

Kwa kiasi fulani kitu ambacho Google wamekiongeza kwenye Google Map vinakaribiana na kile ambacho WhatsApp wamekifanya hivi karibuni kwa kuongeza kipengele cha Live Location na kuweza kuwaambia wengine mahali ulipo.

Vyanzo: Gadgets 360, Android Central

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com