Google yazuia watu kusema ya moyoni

0
Sambaza

Google ni moja ya makamuni makubwa sana na yanayoheshika duniani kutokana na kujenga uaminifu kati yake na wateja wa Google waliotapakaa dunia nzima.

Kuna makampuni mengi tu ambayo yanaitumia uwanja wa Google ambao unaruhusu wafanyakazi wa sasa/zamani kuweza kutoa maoni kuhusu kampuni wanayofanya kazi au walipokuwa wanafanya kazi huko nyuma. Google imeamua kuanza mwaka kwa kurekebisha sera zake kwenye kipengele cha kutoa maoni kuhusu kampuni fulani.

Google imeweka katazo kwa yeyote yule ambaye ana maoni hasi kuhusu kampuni anayofanya kazi/alikwishawahi kufanya kazi miaka ya nyuma.

Kupitia kipengele cha Google My Business huko nyuma kiliwezesha watu kutoa maoni yao kuhusu kampuni/shirika fulani lakini hali imekuwa ni tofauti tangu Januari Mosi 2018 kwani haiwezekani tena mtu kuweza kuandika maoni hasi kuhusu kampuni anayotaka kuiongelea na katika kusisitiza hilo kuna watu tayari wamefungiwa uwezo wa kusema ya kwao.

Google na maoni ya wafanyakazi: Takwimu za watu zinjazojumuisha maoni chanya na hasi kwenda kwa kampuni.

Maamuzi ya Google kuzuia watu kusema ya moyoni kunalenga kulinda heshima ya kampuni husika kutokana na ukweli kwamba kile kinachosemwa kinaweza kuharibu/kuwatengenezea sifa nzuri kampuni inayozungumziwa.

SOMA PIA:  Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

Hali ilivyo hivi sasa kampuni/mashirika yanaweza kuwasiliana na Google moja kwa moja na kuomba kuondolwa maoni yote ambayo yanaonekana kuwa ni mabaya/yanayoweza kuharibu picha ya kampuni husika kwa wateja na watu mbalimbali.

Chanzo: Gadgets 360

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com