Gorilla Glass 5; Teknolojia mpya ya Vioo Kufanya Simu yako Kuwa ngumu zaidi

0
Sambaza

Teknolojia ya vioo ya Gorilla Glass ndio teknolojia inayotumika zaidi katika ‘display’ za simu, tableti na vifaa vingine janja ili kuepusha kuvunjika pale vinapodondoka.

Gorilla Glass Corning Inc

Muonekano wa kioo cha Gorilla Glass, kampuni ya Corning Inc inatengeneza teknolojia ya vioo hivi tokea mwaka 1962

Kampuni inayotengeneza vioo hivyo, Corning, imekuja na toleo jipya linalosemekana kuwa ni salama zaidi. Kampuni hiyo ya jijini New York nchini Marekani inadai vioo vyake hivi vipya vya Gorilla Glass vinanguvu ya zaidi ya mara nne ukilinganisha na vya wapinzani wake.

Inasemekana teknolojia ya Gorilla Glass inatumika katika zaidi ya vifaa bilioni 4.5 tokea mwaka 2007, wateja wakuu wa kampuni hiyo ya Corning ni pamoja Samsung, Apple, Motorola, LG, HP na makampuni mengine.

SOMA PIA:  Rudisha mafaili yaliyojificha kwenye memori kadi yako!

Inasemekana kwa toleo hili la 5 la Gorilla Glass basi uwezekano wa simu kutovunjika kioo pale ikidondoshwa kutoka umbali wa mabega au kiuno cha mtumiaji hadi chini unakuwa mkubwa sana..pia ni vigumu zaidi kioo kukwanguliwa na kitu.

Majaribio ya kudodosha yakifanyika, picha na Corning.

Data kutoka utafiti mmoja wa kimataifa unaonesha ya kwamba takribani asilimia 85 ya watumiaji wa simu janja washaangusha simu janja zao angalau mara moja kwa kipindi cha mwaka mmoja….na asilimia 55 washaangusha kwa mara tatu au zaidi kwa kipindi hicho hicho.

SOMA PIA:  Mapendekezo ya Apple kuhusu kuja na emoji zinazohusu walemavu

Inategemewa muda si mrefu simu janja za hadhi ya juu kutoka makampuni makubwa zitakuja na toleo hili la kisasa la Gorilla Glass.

Je wewe unakubali ya kwamba kuvunjika kwa vioo vya simu ni moja kati ya tatizo kubwa zaidi kwa wamiliki wa simu janja? Unachukua hatua gani kuhakikisha simu yako inaendelea kuwa salama?

Chanzo: BBC, DenverPost

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com