Hadithi App: App Inayokuletea Stori Mbalimbali kwa Wepesi kwenye Simu Yako

1
Sambaza

Je wewe unakipaji cha uandishi wa stori mbalimbali? Au ni mpenzi wa kusoma stori mbalimbali? Basi Hadithi app ni app ya kudownload.

Ni app ya kitofauti sana na uwezi kubisha ya kwamba ni app yenye umuhimu kwa watu wote wanaopenda kusoma hadithi (stori) za kiswahili, na waandishi pia – kwani kupitia app hii wote wawili (watunzi na wasomaji) wanaunganishwa kwa urahisi sana.

Hadithi App

Muonekano wa Hadithi App

Nimeitumia app hii kwa zaidi ya wiki 3 sasa na huu ndio mtanzamo wangu;

  • Waandishi wanazidi kuongezeka na stori mpya pamoja na miendelezo inaendelea kuwekwa.
  • Na nimependa kuona kukiwa na stori mpya n.k unapata taarifa kupitia eneo la ‘notification’
  • Ni app isiyo na muda mrefu sana ila inaonekana tayari imepata wasomaji wengi kwani kupitia data zinazoonekana kwenye kila stori – imetazamwa mara ngapi – zinaonesha watu wanazisoma hadithi sana
SOMA PIA:  Wasimamizi wa makundi Whatsapp kukiona cha moto India

Mara unapoifungua unakutana na eneo linalokuonesha Stori Mpya, chaguo la pili ni Makundi (yaani aina za stori), na mwisho ni waandishi.

Stori katika app hii zimegawanywa katika makundi ya;

  • Maisha
  • Mapenzi
  • Chombezo
  • Upelelezi
  • Uchawi
  • Mapigano
  • Vichekesho

 

Lakini katika muda mdogo niliotumia naona stori za mapenzi ndio zinapendwa zaidi na wasomaji…. 🙂

App hii kwa sasa inapatikana katika soko la Google Play | Hadithi App , ipakue na utuambie mtazamo wako juu ya app hii kwenye eneo letu la comment. 

SOMA PIA:  Hivi karibuni utaweza kufuta ujumbe uliokwishatumwa WhatsApp

Je unaijua app nyingine ya kitanzania inayovutia na ungependa tuipaishe pia kupitia TeknoKona? Usisite kuwasiliana nasi au kuwaambia wengine kupitia eneo la comment.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com