Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Halotel imesema hivi sasa wateja wake wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, huku ikiwa imepunguza gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.
Kuondolewa kwa makato hayo inatafsiriwa na kampuni kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu, taarifa ilisema.
Kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao huo, hasa walioko maeneo ya vijijini kufanya miamala ya simu na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kupata kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.
Aidha, licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha, huduma ya kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine imepunguzwa gharama ili iwe rahisi zaidi kwa wateja wanaotuma pesa kwenda mitandao mingine ya simu.