Mtandao wa KickassTorrents ambao ni mmoja kati ya mitandao mikubwa ya kusambaza filamu, miziki na program za kompyuta umefungwa leo na pia Artem Vaulin (30) anayetuhumiwa kuwa ndiye mmiliki wake amekamatwa na maafisa wa Marekani akiwa nchini Poland.
Anuani nyingi ambazo zilikuwa zinatumiwa na mtandao huu zimeanza kufungwa ingawa zipo baadhi mpaka wakati wa kuandika makala hii zilikuwa zinafanya kazi. Pamoja na kuzifunga anuani za mtandao huo maafisa hawa pia wanafanya mpango wa kumsafirisha Artem Vaulin kwenda marekani ili akashitakiwe huko.
Kwa wasioijua KickassTorrents (Torrenting)
Torrenting ni itifaki ama protocol ama unaweza kuuita njia ya kushirikishana mafaili kati ya kompyuta na kompyuta, KickassTorrents na mitandao mingine ya kiharamia inatumia teknolojia hii kusambaza nakala hata za filamu miziki na programu za kompyuta ambazo zina haki miliki bila ya gharama yeyote.
Soma Pia – Fahamu jinsi ya kudownload vitu kupitia mfumo wa Torrent
Kwa wapenda filamu na miziki hapa ndio imekuwa mahara pa kupata mahitaji yao ya muziki filamu na hata programu za kompyuta huduma hizi zinatolewa na mitandao mingi lakini mpaka miaka ya karibuni KickassTorrents ilianza kushika kasi baada ya mtandao uliokuwa juu kupata matatizo kama haya yaliyowakuta KickassTorrents.
Makosa aliyoyafanya Artem Vaulin yaliyomfanya ashtukiwe na maafisa wa Marekani na kukamatwa
- Kwanza Artem alitumia anuani yake katika soko la muziki la iTunes anuani hii ndiyo aliyokuwa anatumia katika kuendesha mtandao huu.
- Alikuwa anatumia kompyuta moja kuingia iTunes na pia katika ukurasa wa Facebook wa Kickasstorrents kitu ambacho kilithibitisha kwamba lazima mtumiaji wa akaunti ya iTunes atakuwa ndiye mmiliki wa mtandao huu
- Username “Nike” aliyokuwa anaitumia kuingilia katika servers za KickassTorrents ndiyo ilikuwa username katika mtandao wake wa kuchat kipindi cha nyuma.
- Artem alikuwa amejiandikisha iTunes kwa barua pepe ya tirm@me.com lakini inajulikana wazi kwamba “tirm” ni username ya mtawala (administrator) wa Kickass
Pengine kukamatwa kwa Artem Vaulin kwa namna moja kunaweza kugeuza mtazamo wa watu kwa kampuni ya Apple ambayo ilitoa taarifa za kijana huyo baada ya kuombwa na maofisa usalama wa Marekani. Miezi michache nyuma ilionekana kinara wa kutunza siri za wateja wake.
One Comment
Comments are closed.